NDALICHAKO ATOA MAAGIZO BODI MPYA YA VETA

Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) imeagizwa kuanza mara moja kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake umekuwa ukisuasua kwa muda mrefu huku kukiwa na fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji miradi hiyo.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na wakati akizindua Bodi Mpya ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) Jana Jijini Dar es Salaam.
Prof. Ndalichako ameshangazwa na kitendo hicho cha ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi hiyo huku kukiwa na shilingi takribani bilioni 14.5 zilizotengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/207 kwa ajili ya kazi hizo.
“Inasikitisha kuona kuwa tunakaribia robo ya mwisho ya mwaka wa fedha 2016/2017, huku karibu miradi yote ya maendeleo haijaanza kutekelezwa,isipokuwa ile tu ya kujengea uwezo na siyo ya ujenzi wa VETA ambazo ndiyo hitaji kubwa kwa sasa.”amesema Profesa Ndalichako.
Aidha, Ndalichako ameongeza kuwa Bodi hiyo inapaswa kuanza kazi mara moja ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua watendaji watakao bainika kuhusika katika ucheleweshaji wa kuanza kwa miradi hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Peter Maduki amempongeza Waziri Ndalichako kwa kuwa muwazi katika kuelezea kutoridhishwa na udhaifu katika utendaji kwa baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na kuahidi kushughulikia suala hili huku akiwataka wajisahihishe badala ya kusubiri kuwajibishwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post