NDEGE ZA KIVITA ZA KIMAREKANI ZAENDELEA KUISAIDIA SAUDI ARABIA KUWAUA WAYEMENI

Ndege za kivita za Marekani zisizokuwa na rubani zimeendelea kuisaidia Saudia katika kuwaua Wayemen na mara hii zimeshambulia maeneo 30 tofauti ya mkoa wa Al Bayda, katikati mwa nchi hiyo.
Mashuhuda katika mkoa huo wa Al Bayda wamesema kuwa, ndege hizo za Marekani zisizo na rubani zimetekeleza hujuma katika maeneo ya kusini na mashariki ya mkoa huo na kusababisha hasara kubwa. Kwa mujibu wa ripoti hiyo hujuma hiyo imetekelezwa katika hali ambayo Jumatano usiku ndege kadhaa za Marekani zilionekana zikiruka kwa pamoja katika wilaya ya As Sawma'ah mkoani al Bayda.
Kabla ya hapo pia yaani sawa na tarehe 19 Januari mwaka huu, ndege hizo za Marekani zilishambulizi eneo la Wadi Said ambapo makumi ya familia za Wayemen zilikuwa zimetia kambi na kusababisha karibu watu 50 wakiwamo watoto na wanawake kuuawa. Inafaa kuashiria kuwa, Saudia kwa kushirikiana na Marekani, Israel, Uingereza na baadhi ya nchi za Kiarabu, ilianzisha hujuma za kila upande dhidi ya Yemen hapo mwezi Machi mwaka 2015 kwa lengo la kumrejesha madarakani kibaraka wake, Abdrabbuh Mansur Hadi rais wa zamani wa Yemen aliyejiuzulu wadhifa huo na kukimbilia Riyadh.
Hujuma hizo za Saudia na waitifaki wake zimesababisha zaidi ya watu elfu 38 kuuawa na kujeruhiwa sambamba na kuharibu miundombinu kama vile shule, hospitali, madaraja, ofisi za serikali na mashirika tofauti, barabara na makazi ya raia. Aidha zaidi ya watu milioni mbili wamekuwa wakimbizi hadi sasa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post