NEEMA WAMBURA AELEZEA HALI YAKE BAADA YA KUPEWA MSAADA WA MATIBABU NA RAIS MAGUFULI

Mgonjwa Neema Wambura ambaye alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) amemshukuru Rais John Pombe Magufuli baada ya afya yake kuimarika na kuruhusiwa leo kurejea nyumbani.
Neema amemshukuru rais kwa kumwezesha kupata matibabu tangu alipofikishwa katika hospitali hiyo Februari 23, mwaka huu.
“Namuomba Mwenyezi Mungu amuepushe Rais Magufuli na mambo mabaya yote. Sasa nipata nguvu, nina furaha na naoga mwenyewe tofauti na awali,” amesema Neema.
Pia, Neema amewashukuru madaktari na wauguzi wa Muhimbili kwa kumpatia huduma bora na kumwezesha kupona majeraha ya moto.
Neema ambaye ni Mkazi wa Mkoa wa Mara alimwagiwa maji ya moto na mumewe wakati alipokuwa akichemsha maji kwa ajili ya kupika ugali na kuungua sehemu ya kifuani, shingo na mkono.
Mkuu wa Idara ya Upasuaji na Daktari Bingwa wa Upasuaji, Dk Ibrahim Mkoma  amesema afya ya Neema inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji sehemu ya shingoni ili kutenganisha shingo na sehemu ya kifua na kuziba majera ya moto.
“Neema anaendelea vizuri sasa anaweza kunyanyua shingo vizuri kabla ya hapo alikuwa hawezi kuinyanyua wala kuizungusha.”
Ameruhusiwa kutoka Hospitalini hapo ambapo Daktari amesema kwa mara ya kwanza walimpokea mwaka 2015 akiwa na majeraha hayo ya moto. Kazi kubwa walioifanya mi kutemgemisha shingo, kifua na mkono vilivyokuwa vumeshikana kutokana na moto huo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post