NJIA SITA ZA KUTUMIA MAJI KUJIKINGA NA MAGONJWA MBALIMBALI

Watu wengi wamekuwa wavivu wa kunywa maji, hawajui kuwa maji ni muhimu sana katika mwili na yanahitajika kwa kiwango kikubwa. Wengi hawajui kuwa maji ni tiba ya maradhi mengi. Ili maji yawe tiba ya magonjwa, ni lazima ufuate kanuni ya namna ya kuyatumia.
Maji huwa na faida nyingi. Zifuatazo ni baadhi ya faida za kunywa maji kwa wingi.
Maji husafisha figo. Figo kuwa na uchafu ama vimawe vidogo vidogo husababishwa na kutokunywa maji ya kutosha. Maji huyeyusha takataka zote zonazojiunda kutengeneza vijimawe katika mkojo. Hivyo kunywa maji mengi kutasaidia kusafisha figo zako.
Maji huponya maambukizi ya njia ya mkojo. Kadiri unavyokunywa maji mengi, ndivyo unavyokojoa zaidi. Kunywa maji kwa wingi kutasaidia kuondoa bakteria katika kibofu chako cha mkojo.
Maji husaidia kutuliza homa. Homa ni kuongezeka kwa kiwango cha joto mwilini kinachosababishwa na sababu mbalimbali. Kunywa maji mengi kutakusaidia kupunguza joto hilo kupitia mkojo. Kama una homa kunywa maji mengi na utapata ahueni.
Maji husaidia kupunguza uzito wa mwili. Kunywa glasi moja au mbili muda mchache kabla ya kula kutakufanya ule chakula kidogo. Kwa vile maji hayana kalori yoyote, itakupunguzia uwezekano wa kunenepa.
Maji huifanya ngozi yako kuwa laini na nyororo. Maji yatasaidia kuilainisha ngozi yako na kukufanya uwe na macho ang’avu kama tu utayanywa kwa wingi kila siku.
Ushauri wa kiafya wa namna nzuri ya kunywa maji
Kunywa maji punde tu unapoamka. Mwili wako hupoteza kiwango kikubwa cha maji unapokuwa umelala, hivyo jitahidi kunywa maji kabla ya kwenda kulala na baada ya kuamka. Unapokunywa maji asubuhi, husaidia kuondoa sumu zote zilizotengenezwa mwilini ulipokuwa umelala.
Jitahidi kunywa glass 8 mpaka 12 kwa siku. Kulingana na kliniki ya afya ya Mayo, mtu mwenye uzito wa kilo 55 anatakiwa kunywa maji glass 8 wakati mtu mwenye uzito wa kilo 87 anatakiwa kunywa maji glass 12 kwa siku. Inabidi kuhakikisha kuwa rangi ya mkojo inakuwa nyepesi. Unashauriwa kutokunywa zaidi ya glass 16 kwa siku.
Usisubiri mpaka kiu ikupate ndipo unyewe maji. Wakati unapohisi kiu, inawezekana umeshapunguza glass 2 katika kiwango cha maji kinachotakiwa mwilini. Wazee huwa hawapatwi na kiu mara kwa mara, kwahiyo wanahitajika kunywa maji hata pasipo kuhisi kiu.
Kunywa maji mengi unapokuwa mgonjwa. Hata kama hujisikii kunywa maji, kiukweli unahitaji kunywa maji zaidi ili kuusaidia mwili wako kupambana na maradhi. Maji yanapopungua mwilini mwako, ndivo ugonjwa unavopata nguvu ya kukutesa.
Kunywa maji mengi kama hali ya hewa ni ya joto. Watu wanaoishi katika maeneo yenye joto kama Dar es salaam, wanatakiwa kunywa maji kwa wingi. Watu hawa wako katika hatari ya kupata matatizo ya figo kama hawatakunywa maji kwa wingi ukilinganisga na watu wanaoishi katika maeneo yenye baridi kama vile Iringa na Mbeya.
Kunywa maji, na siyo vinywaji baridi, vileo ama kahawa. Baadhi ya wataalamu wanaamini kuwa chai, soda na kahawa vinaweza kuongeza kiwango cha maji mwilini. Ingawa vinywaji hivyo vina kiwango kikubwa cha kaboni na sukari ambayo inaweza kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari na mifupa. Utafiti unaonyesha kuwa watu wanaokunywa vikombe 6 vya kahawa kila siku, huongeza maji mwilini kwa kiwango kidogo sana. Pombe ndiyo mbaya zaidi kwani hukusababisha ukojoe sana na kupoteza kiwango kikubwa cha maji mwilini.
Kunywa maji kwa wingi kama unafanya mazoezi. ukiwa unafanya mazoezi, unatakiwa kunywa maji kwa wingi kwa kuwa unakuwa umepoteza kiwango kikubwa cha maji mwilini. Ongeza nusu lita zaidi kwa kila nusu saa mpaka saa moja ya kufanya mazoezi. Kula ndizi kutakusaidia kuongeza kiwango cha madini ya potassium mwilini.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post