OZIL, DRAXLER, GOMEZ KUIKOSA ENGLAND

Mabingwa wa soka duniani, timu ya taifa ya Ujerumani watawakosa baadhi ya wachezaji wao katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya England ambao umepangwa kuchezwa leo.
Kiungo Mesut Ozil, mshambuliaji wa pembeni Julian Draxler na mshambuliaji wa kati Mario Gomez wametajwa na kocha mkuu wa kikosi cha Ujerumani Joachim Loew, wataukosa mchezo huo.
Loew amesema wachezaji hao wana majeraha madogo madogo, na itawachukua siku kadhaa kupatiwa matibabu kabla ya mchezo kuwania kucheza fainali za kombe la dunia dhidi ya Azerbaijan utakaochezwa mwishoni mwa juma hili mjini Baku.
“Ozil, Julian Draxler na Mario Gomez hawatokua sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya England.” Alisema Loew
Kocha huyo aliyekiongoza kikosi cha Ujerumani kutwaa ubingwa wa dunia katika fainali za mwaka 2014 zilizofanyika nchini Brazil, amesema Gomez, Ozil na  Julian Draxler wanasumbuliwa na majeraha ya misuli ya paja.
Kabla ya taarifa za wachezaji hao watatu kutolewa na kocha huyo kupitia mkutano na waandishi wa habari, tayari ilikua inafahamika Ujerumani itamkosa mlinda mlangi wake mahiri Manuel Neuer ambaye ni majeruhi, na nafasi yake itajazwa na mlinda mlango wa Paris Saint-Germain Kevin Trapp.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post