PICHA: MWANAMITINDO AGONGWA NA TRENI AKIPIGA PICHA

Mwanamitindo Fredzania Thompson aliyekuwa na umri wa miaka 19 amefariki dunia baada ya kugongwa na treni huko Texas, Marekani wakati akipigwa picha.
Mamlaka zinasema kuwa Thompson alikuwa amesimama katikati ya reli  pale ambapo treni ya BNSF ilipokuwa inakaribia. Alitoka kwenye reli lakini hakugundua kuwa treni ya umoja wa Pasifiki ilikuwa ikija kutokea upande mwingine wa reli na akagongwa.
Image result for Fredzania Thompson
Hakamie Stevenson ambaye ni baba wa binti huyo alieleza kuwa binti yake alisoma chuo cha Blinn kilichopo Bryan, Texas na alitamani kujiingiza katika masuala ya mitindo. “Hicho ndicho alichokuwa anakitaka haswa. Na ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza siku hiyo aliyogongwa na treni.” Alisema Baba wa Thompson
Aliyekuwa akipiga picha hizo hakuumia. Justin LEETH, mkuu wa polisi wa Idara ya Polisi Navasota aliiambia CNN kuwa”Kwa sasa bado hatujagundua kama kuna hila yoyote iliyosababisha kifo chake,”
Mchumba wake alieleza kuwa wiki mbili zilizopita Thompson alimwambia kuwa ni mjamzito.
“Alikuwa akiwasaidia sana ndugu zake, na alihakikisha kuwa kila kitu kinafanyika kwa tahadhari, alikuwa kiongozi mzuri.” Alisema mama yake.
thompsthomp2

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post