PICHA: NAPE AMKABIDHI RASMI OFISI WAZIRI DKT MWAKYEMBE

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Mtama, Nape Moses Nnauye leo amemkabidi rasmi ofisi waziri mpya wa wizara hiyo, Dkt Harrison George Mwakyembe.
Tukio hili linatokea ikiwa ni takribani wiki moja tangu Rais Dkt Magufuli alipotengua uteuzi wa Nape Nnauye na kumteua Harrison Mwakyembe kujaza nafasi hiyo. Aidha, Rais Magufuli alimteua Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria akijaza nafasi iliyoachwa wazi na Harrison Mwakyembe.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, haikueleza sababu ya Rais Dkt Magufuli kumvua uwaziri Nape Nnauye ikiwa ni saa chache tu tangu alipopokea ripoti ya uvamizi wa kituo cha runinga cha Clouds, tukio lililofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Hapa chini ni picha za matukio ya makabidhiano ya ofisi leo;
IMG_-s68vbwIMG_-wxzoe2IMG_r83wzk

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post