POLISI ‘WATINGA’ NYUMBANI KWA GWAJIMA, MWENYEWE AFUNGUKA

Askari wa Jeshi la Polisi, jana walifika nyumbani kwa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kufanya uangalizi.
Taarifa zilizotolewa na Askofu huyo zimeeleza kuwa askari hao waliofika nyumbani kwake walitaka kuingia ndani lakini walizuia na walinzi wake baada ya kuhojiwa na kubainika kuwa hawakuwa na nyaraka za kisheria zinazowapa mamlaka ya kuingia au kufanya upekuzi.
Kiongozi huyo wa dini aliliambia gazeti moja la kila siku kuwa baada ya askari hao kuhojiwa na walinzi walieleza kuwa wametumwa na Afande Kingai, hali iliyosababisha mwanasheria wake kumpigia simu Afande aliyetajwa ambaye ameelezwa kuwa ndiye aliyepewa jukumu la kuwafuatilia watu waliokumbwa na tuhuma za dawa za kulevya.
“Afande Kingai amemueleza mwanasheria wangu kuwa wamekuja kwa ajili ya observation (uangalizi) tu, kwa hiyo mwanasheria wangu akasema kama ni observation tu tusiwaruhusu kuingia ndani kwa sababu sheria ya hivyo hakuna,” Gwajima anakaririwa na Mtanzania.
Alisema baada ya kuelezwa hayo waliwazuia askari hao kuingia ndani. Hivyo, baadae waliamua kuondoka.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alipotafutwa kutolea ufafanuzi suala hilo, simu yake iliita bila majibu.
Gwajima alikuwa miongoni mwa wanatu 65 waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwa wanatuhumiwa kujihusisha na matumizi, biashara ya dawa za kulevya. Hata hivyo, baada ya kufanyiwa upekuzi na vipimo na mkemia mkuu wa Serikali, Askofu huyo alitangaza kuwa hakukutwa na hatia yoyote.
Wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mfanyabiashara maarufu ambaye pia ni Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusufu Manji.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post