POLISI WATOA ORODHA YA MAKOSA BARABARANI NA ALAMA ZITAKAZOKATWA KWENYE LESENI

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limetoa orodha ya makosa yatakayopelekea dereva wa chombo cha moto kupunguziwa alama katika leseni yake pindi atakapokamatwa ametenda kosa hilo.
Kila leseni moja huwa na jumla ya alama 15, hivyo kadiri unavyooendelea kutenda makosa na kukatwa ndio leseni yako itakavyokua inafikia mwisho wa matumizi.
Hapa chini ni baadhi ya makosa hayo na alama zitakazokatwa.
Makosa utakayokatwa alama moja.
 1. Kutokuwa na, au kutobandika alama za utambulisho
 2. Makossa ya ubovu wa gari (roadworthiness)
 3. Kuendesha taratibu sana
 4. Kumzuia dereva wa gari
 5. Kutokuwa na reflector
 6. Kushindwa kusimama
 7. Gari kuwa na tairi mbovu
 8. Kusababisha kelele za kubwa na gari kutoa moshi mwingi
 9. Kuendesha gari la mtu bila ridhaa yake
 10. Kuendesha gari la mtu bila ridhaa yake
Makosa utakayokatwa alama tatu
 1. Kuendesha gari bila kusajiliwa
 2. Gari la mafunzo ya udereva kutokuwa na alama za utambulisho
 3. Kuendesha bila kuwa na leseni
 4. Kukiuka maelekezo ya uendeshaji gari barabarani
 5. Kutofunga mkanda au kuvaa helmeti
 6. Kuendesha upande hatari
 7. Kupakia mtu Zaidi ya mmoja kwenye pikipiki (mishikaki)
 8. Kutumia gari ya abairia kubeba mizigo
 9. Kutoegesha kushoto
 10. Kushindwa kutii sheria za barabarani
 11. Kupakia kwa hatari
 12. Kuegesha kwenye njia za waenda kwa miguu
 13. Kuzuia au kuingilia msafara rasmi
 14. Kushindwa kupunguza mwanga wat aa usiku
Makosa utakayokatwa alama tano.
 1. Kuendesha bila kuwa na sifa za udereva
 2. Kuzidisha spidi
 3. Kuendesha ukiwa umekunywa kilevi/madawa
 4. Kuovateki vibaya
 5. Kutosimama kabla ya zebra
 6. Kutoheshimu taa na michoro barabarani
 7. Kutokuwa na bima hai
 8. Kuzidisha abiria
 9. Kubeba abiria kwenye gari lisiloruhusiwa
 10. Kutosimama kwenye vivuko vya reli
 11. Uendeshaji wa hatari
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post