PROFESA MBARAWA AZINDUA MFUMO WA KUHAMA MTANDAO

Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliani, Profesa Makame Mbarawa amezindua rasmi huduma ya kuhama mtandao (MNP) na kuwaonya watoa huduma (mitandao) watakaowakwamisha wateja wao kuhama.
Profesa Mbarawa amesema huduma hiyo imeanzishwa ili kumpa uhuru mtumiaji wa kuchagua huduma bora, jambo litakalowafanya watoa huduma kuboresha huduma zao.
Amesisitiza kwamba matumizi ya mfumo wa MNP yatafanikiwa kwa sababu ni rahisi ukilinganisha na ule wa kuhama kutoka analogi kwenda digitali uliofanyika miaka michache iliyopita na kuipa sifa Tanzania.
"Tunataka wananchi wajue kwamba huduma hii ni bure na wasilazimishwe kuhamia mtandao fulani kwa kushinikizwa. Hii ni Huduma ya hiari na hatutasita kuchukua hatua kwa kampuni ya simu itakayokiuka utaratibu huu," amesema.
Huduma hii ya MNP katika Afrika inatumika katika nchi nane, lakini kwa Afrika Mashariki inapatikana Kenya pekee na Tanzania leo inakuwa ya pili wakati nchi za Rwanda na Uganda wakiwa kwenye mchakato huo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post