PSG WAMSHTAKI MWAMUZI DENIZ AYTEKIN

SHARE:

Klabu bingwa nchini Ufaransa PSG imetuma taarifa yenye kurasa tano ya malalamiko kuhusu mchezo wa hatua ya 16 bora wa ligi ya mabingwa ba...

Klabu bingwa nchini Ufaransa PSG imetuma taarifa yenye kurasa tano ya malalamiko kuhusu mchezo wa hatua ya 16 bora wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya FC Barcelona, uliopigwa juma lililopita kwenye uwanja wa Camp Nou.
PSG wamelalamikia maamuzi mabovu ambayo wanadai yalichangia ushindi wa mabao sita kwa moja, ulioivusha FC Barcelona na kutinga kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Mwamuzi Deniz Aytekin ametajwa katika malalamiko hayo ya PSG, kama kichwa cha matatizo yote ambayo yalionekana kwenye mchezo huo ambao kwa asilimia kubwa uliwashangaza wadau wa soka ulimwenguni, kutokana na hitaji la FC Barcelona la kusaka ushindi wa zaidi ya mabao manne kukamilika.
Uongozi wa PSG umeeleza kusikitishwa maamuzi ya mwamuzi huyo kutoka nchini Uturuki, na unahisi kulikua na sababu za nyuma ya pazia, ambazo zilimsukuma kutoa maamuzi ya utata wanayodai yaliisaidia FC Barcelona kupata ushindi wa mabao sita kwa moja.
Sehemu ya malalamiko ya PSG ambayo yameorodheshwa kwenye taarifa yenye kurasa tano iliyowasilishwa huko UEFA, inadai katika mchezo huo kiungo kutoka nchini Argentina Javier Mascherano aliunawa mpira dakika 10 kabla ya mchezo kumalizika, baada ya kupigwa na kiungo Julian Draxler kuelekea katika eneo la hatari la FC Barcelona, na mwamuzi Deniz Aytekin alishindwa kupuliza kipyenga kwa kuashiria kosa hilo limefanyika.
Kadi ya pili ya GERARD PIQUE – PSG wamedai kuwa, beki huyo kutoka nchini Hispania alipaswa kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kisha nyekundu katika dakika ya 41, kufuatia kitendo cha kumvuta jezi kwa makusudi mshambuliaji wao Edinson Cavani, lakini haikuwa hivyo.
Penati iliyokwamishwa wavuni na Neymar – Hapa mwamuzi Aytekin kuizawadia penati ya upandeleo FC Barcelona kwa madai ya beki wa upande wa kulia wa PSG Thomas Meunier alimfanyia madhambi mshambuliaji huyo kutoka Brazil, jambo ambalo linapingwa na mabingwa hao wa Ufaransa.
Kujiangusha kwa Luis Suarez – Luis Suarez anadaiwa kujiangusha katika eneo la hatari kwa kisingiozio cha kufanyiwa madhambi na Marco Verratti. Lakini PSG wamesisitiza tukio hilo halikua na uhalali wa kusababisha adhabu.
Pique Kuushika Mpira – PSG wamedai kuwa mshambuliaji wao Angel di Maria alishindwa kufikia lengo la kupiga mpira uliokua unaelekea langoni mwa FC Barcelona, baada ya Pique kuushika mpira kwa makusudi katika eneo la hatari, na mwamuzi hakuchukua maamuzi yoyote.
Penati Ya Suarez – PSG wamelalamika kwa kueleza mkwaju wa penati uliopigwa na Neymar baada ya Luis Suarez kuonekana aliangushwa kwenye eneo la hatari, haikuwa sahihi kufuatia beki wa mabingwa hao wa Ufaransa Marquinhos kuanguaka sambamba na mshambuliaji huyo wa Uruguay.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: PSG WAMSHTAKI MWAMUZI DENIZ AYTEKIN
PSG WAMSHTAKI MWAMUZI DENIZ AYTEKIN
https://2.bp.blogspot.com/-JqUKMiVJgo0/WMkGFKyV8KI/AAAAAAAAX9g/yZ6j2ioQMLUsi9rrqntqvstlmDsz-GnYwCLcB/s1600/Deniz-Aytekin.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-JqUKMiVJgo0/WMkGFKyV8KI/AAAAAAAAX9g/yZ6j2ioQMLUsi9rrqntqvstlmDsz-GnYwCLcB/s72-c/Deniz-Aytekin.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/psg-wamshtaki-mwamuzi-deniz-aytekin.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/psg-wamshtaki-mwamuzi-deniz-aytekin.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy