RAIS DKT. MAGUFULI AMTAKA MAKONDA KUCHAPA KAZI

Rais Dkt. John Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuendelea kuchapa kazi na kwamba yeye hafanyi kazi kwa kusikiliza maneno ya watu kwenye mitandao kwasababu yeye ndiyo Rais wa nchi hii.
Ameyasema hayo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu za Ubungo (Ubungo Fly Over) jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanaingilia majukumu yake wakati yeye ndiyo mwenye maamuzi na kwamba hapangiwi kazi ya kufanya kwa sababu anajiamini.
Aidha, Rais Magufuli  amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo badala ya kupoteza muda mwingi kufuatilia udaku kwenye mitandao.
“Watu wa Dar es Salaam tumejielekeza sana kwenye masuala ya udaku ambao hausaidii maendeleo. Udaku ambao haumalizi hata foleni ya Dar, ningefurahi sana huko kwenye mitandao kama tungekuwa tunajadili jinsi ya kufanya mambo ya maendeleo, Mimi sionyeshwi njia ya kupita na mtu, njia ya kupita tayari nilishaonyeshwa na ilani ya chama changu,”amesema Rais Magufuli.
Vile vile Rais Magufuli amesema kuwa, yeye anaandikwa sana kwenye mitandao kamwe hatoweza kujiuzulu kwaajili ya kuandikwa bali ataongeza kasi ya kufanya kazi.
Hata hivyo, amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanadiriki hata kumpangia nini cha kufanya, wakati huo ndio wanaharibu kwa sababu wanapanga vitu visivyo vya msingi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post