RAIS DKT. SHEIN AMTAKA MAALIM KUTOVUNJA SHERIA ZA NCHI

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein amemtaka Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuikosoa Serikali yake pasipo kuvunja sheria za nchi.
Ameyasema hayo Ikulu ya Zanzibar wakati akiadhimisha mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani kupitia uchaguzi wa marudio wa Machi 20 mwaka jana, Dkt Shein amesema kuwa, Maalim Seif Hamad ana uhuru wa kusema akitakacho wakati wowote, lakini asitumie lugha za matusi.
Aidha, Dk Shein amesema kuna maneno mengi yamekuwa yakisemwa mitaani juu ya kuwapo kwa Serikali nyingine badala ya anayoiongoza, kauli ambapo amesemakuwa kauli hizo hazina mashiko.
Hata hivyo, Shein amezitaja njia za kupata Serikali kuwa ni mbili tu duniani kote, ambapo amesema kuwa moja ni ya kupigiwa kura na nyingine ni ya kufanya mapinduzi kwa upande unaohisi  umeonewa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post