RAIS MAGUFULI AMPIGIA SIMU DIAMOND PLATNUMZ. FAHAMU WALIYOZUNGUMZA

Rais Dkt John Pombe Magufuli leo asubuhi amepigia simu na kumpongeza mwanamuziki Diamond Platnumz kwa namna anavyojituma katika kuiinua sanaa ya Tanzania.
Rais Magufuli amepiga simu hiyo mapema leo asubuhi ambapo Diamond alikuwa katika kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv akitoa maombi yake ambayo angetamani Rais Magufuli afanye ili kuweza kuiinua zaidi sanaa ya Tanzania.

Miongoni mwa mengi ambayo Diamond ameomba kutoka kwa Rais Magufuli ni, kujengwe ukumbi mkubwa wa sanaa ili matamasha makubwa ya muziki yaweze kufanyikia hapa nchini kitu kitakachosaidia kutangaza zaidi muziki wa Tanzania kama ilivyo kwa Afrika Kusini na Nigeria, ambapo tuzo kubwa kama MTV, Channel O hufanyikia.

Ombi lingine kwa Rais Magufuli ni kulindwa kwa kazi sa wasanii. Diamond amesemwa kuwa wasanii wanafanya kazi kubwa sana lakini hawanufaiki nayo kwa sababu mfumo uliopo katika tasnia ya muziki na katika serikali kwa ujumla hauwasaidii wasanii kulika kazi zao. Kwa sasa tumefungua tovuti yetu tunauza nyimbo, lakini kuna watu wanazitoa mule kuanza kuzigawa bure, hili linaturudisha nyuma sana, assema Diamond.

Mimi naiomba serikali ituwekee ulinzi katika kazi zetu kwa sababu kadiri tunavyofaidika sisi ndivyo na serikali inavyozidi kupata mapato. Kama kazi zangu zinaibwa, na serikali haifanyi lolote, nitawezaje kulipa kodi? Kingine kama serikali haiwashughulikii hawa wanaoiba kazi zetu, ndipo pale msanii anakereka hadi unakuta amejichukulia sheria mkononi.
Rais Magufuli alipopiga simu alimpongeza Diamond kwa kupata mtoto wa pili lakini pia kwa kukiri hadharani kuwa ni mwanachama wa CCM.

Kuhusu maombi yake hayo, Rais Dkt Magufulu amesema ameyapokea na atakutana na wahusika kuona ni namna gani anaweza kuyashughulikia.
Katika hatua nyingine, Rais amewapongeza Clouds 360 kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhabarisha umma. Alisema kuwa yeye anawapenda wasanii wote wanaoigiza na wanaoimba na hata kipindi cha SHILAWADU.

Hii ni mara ya tatu Rais Magufuli kupiga simu Cllouds Media.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post