RAIS MUSEVENI ATAKA KUWEKWA KAMERA ZA USALAMA MIJI YOTE

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameagiza kufungwa kamera za usalama katika Jiji la Kampala na katika miji mingine, kufuatia kujirudia kwa matukio ya viongozi kuuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Kauli hiyo ya Museveni ameitoa kufuatia jana kuuwawa kwa kupigwa risasi Mkuu wa Jeshi la Polisi Msaidizi, Andrew Felix Kaweesi na watu wasiojulikana Jijini Kampala, ambapo rais amelaani tukio hilo.

Rais Museveni amesema maafisa ulinzi pamoja na wananchi wanapaswa kuwa imara kuwabaini majambazi hao ambao wameanza kujenga utamaduni wa kuwauwa viongozi wakitumia usafiri wa pikipiki.

Amesema anakumbuka mauaji ya Joan Kagezi, Meja Kigundu pamoja na idadi kadhaa ya masheikh wameuwawa kwa staili kama hiyo, hivyo amewataka wananchi iwapo wakiwashuku watu wenye silaha kutoa taarifa mara moja. 
Mtu akipita huku akiangalia mwili wa AIGP Kaweesi na wasaidizi wake wawili waliouwawa kwenye gari nje kidogo ya Jiji la Kampala
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post