RATIBA YA WANAOKWENDA FAINALI FA CUP YAANIKWA

Chama cha soka nchini England (FA) kimepanga ratiba ya hatua ya nusu fainali ya kombe la FA, baada ya timu nne zilizotinga kwenye hatua hiyo kupatikana.
FA wamepanga ratiba hiyo na kutangaza Aprili 22 na 23 kuwa tarehe maalum za michezo ya nusu fainali itakayoshuhudiwa kwenye uwanja wa Wembley uliopo jijini London.
Mchezo wa kwanza wa hatua hiyo utakuwa kati ya Chelsea ambao wamewavua ubingwa Man Utd usiku wa kuamkia leo, dhidi ya wababe wenzao kutoka jijini London Tottenham Hotspurs walioifunga Milwall mabao sita kwa moja.
Mchezo mwingine wa nusu fainali ambao utachezwa April 23, utakuwa kati ya washika bunduki wa London Arsenal dhidi ya Man City.
Arsenal walitinga hatua ya nusu fainali kwa kuifunga Lincoln mabao matano kwa sifuri, huku Man city wakiitupa nje ya michuano hiyo Middlesbrough kwa kuichabanga mabao mawili kwa sifuri.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post