RC MAKONDA AWAJIBU WANAOSEMA MKEWE SI RAIA WA TANZANIA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  amewajibu wale wote wanaosema kuwa mke wake si raia wa Tanzania na kusema kuwa, hata kama kila siku wataamka na kisa kipya, yeye bado ataendelea kupambana na kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa safi.
Makonda ameyasema hayo leo alipokuwa ibadani katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Usharika wa Kimara ambapo alisema baada ya kuona wamemshindwa sasa wamekuja na kisa cha kudai mkewe si raia halali.
Watu kadha wa kadha kwenye mitandao wamekuwa wakidai kuwa mke wa kiongozi huyo si mtazania ambapo baadhi wamesema kuwa ni raia wa Rwanda.
Kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya, RC Makonda amesema kuwa yeye ataendelea bila kujali watu wanazungumza nini hadi pale Dar es Salaam itakapoacha kuwa lango la kuingiza dawa za kulevya.
Musa alipokuwa anawavusha wana wa Israel katika bahari ya Shamu alipoambiwa na Mungu apige fimbo kwenye maji kisha wavuke, hakwenda kujadiliana na wenzake kuhusu agizo la Mungu bali alipiga fimbo wakavuka. Vivyo hivyo na mimi nasema sitajadiliana na mtu namna ya kuvusha ng’ambo ambapo ni salama, alisema RC Makonda.
Mimi shida yangu si kuwa Mkuu wa Mkoa, lakini shida yangu ni nautumiaje ukuu wangu wa mkoa kutenda mapenzi ya Mungu. Hata nikipewa ukuu wa mkoa kwa siku moja, nitahakikisha natekeleza mapenzi ya Mungu, alisisitza Makonda akizngumza na waumini.
Aidha, Makonda alisema kuwa anafahamu historia ya vita dhidi ya dawa za kulevya ya kuwa hakuna mtu aliyetoka salama. Wote walioanzisha vita hii hawakutoka salama, wengine waliuawa, wengine walifungwa na wengine kupata matatizo mbalimbali sababu wahusika wa biashara hii ni watu wenye nguvu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post