RC SHINYANGA APIGA MARUFUKU KUFANYA SHUGHULI ZA KIBINADAMU KANDO YA VYANZO VYA MAJI

SHARE:

Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack wakati wa kilele c...

Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maji kimkoa.
HOK2
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akipanda mti wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maji kimkoa.
HOK3
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese (katikati) akiongozwa na Kaimu Mhandisi wa Maji, Wilaya, Bernad Bwire (wa pili kushoto) kutembelea bwawa la maji na kupanda miti katika kilele cha Wiki ya Maji. Wengine pichani kushoto ni mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mohamed Mlewa (kushoto) na Kaimu Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari, Steven Cleophace (kulia).
HOK4
Kaimu Mhandisi wa Maji, Wilaya, Bernad Bwire (katikati) akitoa maelezo kwa Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese na viongozi kuhusu mradi wa maji ya bwawa la Sekeididi.
HOK5
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mohamed Mlewa akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maji kimkoa.
HOK6
Wananchi wa kijiji cha Sekeididi Kata ya Sekebugoro wakifuatilia maadhimisho ya Wiki ya Maji kimkoa yaliyofanyika kijijini hapo.
HOK7
Baadhi ya wakuu wa idara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakielekea katika eneo lililotengwa kwa ajili ya zoezi la upandaji miti.
………………………………………………………………..
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack ameagiza wakurugenzi wa mamlaka za Serikali za Mitaa na Maji kuhakikisha hakuna mtu anayefanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji.
Telack alitoa agizo hilo juzi wilayani hapa katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese wakati wa kilele cha maadhimisho Wiki ya Maji yaliyofanyika kijiji cha  Sekeididi.
Aliagiza wakurugenzi hao kuhakikisha vyanzo hivyo vinapandwa miti ili kutunza uoto wa asili ambao mara nyingi huathiriwa na ukame kutokana na kukosekana kwa miti.
Mkuu huyo wa mkoa aliwataka viongozi hao wasimamie utekelezaji wa sheria ya utunzaji wa mazingira ili kunusuru vyanzo vya maji, kwani Serikali inatumia fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maji.
“Utunzaji wa vyazo vya maji ni jambo muhimu katika upatikanaji wa maji na hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kutunza vyanzo vya maji kwa kupanda miti eneo linalozunguka vyanzo.
“Kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, kifungu cha 57, kifungu kidogo cha 1 kinakataza mtu yeyote kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kwenye vyanzo vya maji,” alisema.
Maadhimisho hayo yaliambatana na zoezi la upandaji miti kwenye bwawa la Sekeididi ambalo litakuwa likitoa huduma ya maji kwa wananchi wa maeneo hayo.
Telack aliwataka wananachi kuiunga mkono Serikali katika jitihada zake za kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yao.
Alisema miradi hiyo imeibuliwa na wananchi wenyewe kupitia vikao vyao na hivyo wanapaswa kuendeleza jitihada zao ili kunufaika nayo kwa kuwa wasimamizi wake.
Awali akizungumzia mradi wa ujenzi wa bwawa la maji kijijini hapo, Kaimu Mhandisi wa Maji Wilaya, Bernad Bwire alisema kuwa lina uwezo wa kuhifadhi lita milioni 119.8 za maji.
Alisema bwawa hilo linalojengwa kwa gharama ya sh. milioni 662.4 linatarajiwa kuhudumia wananchi 16,627 wa vijiji vinne vya Bugoro, Ngwashinong’ela na Mwagalankulu katika kata ya Sekebugoro.
Mhandishi Bwire alisema ili kulifanya bwawa lidumu wananchi wamejipanga kuhifadhi mazingira yanayolizunguka kwa kuzuia mifugo kuingia katika eneo la bwawa.
Aliongeza kuwa katika kipindi cha Wiki ya Maji jumla ya miti 230 imeshapandwa na kuwa wanatarajia kupanda mingine 800 zaidi katika eneo la kuzunguka bwawa hilo.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: RC SHINYANGA APIGA MARUFUKU KUFANYA SHUGHULI ZA KIBINADAMU KANDO YA VYANZO VYA MAJI
RC SHINYANGA APIGA MARUFUKU KUFANYA SHUGHULI ZA KIBINADAMU KANDO YA VYANZO VYA MAJI
https://3.bp.blogspot.com/-a0xJ_15yjcs/WNOhs6TetqI/AAAAAAAAYhE/_Oi39tgWLQMu5l5DV_wOnHX2NCcw-TzDwCLcB/s1600/HOK1.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-a0xJ_15yjcs/WNOhs6TetqI/AAAAAAAAYhE/_Oi39tgWLQMu5l5DV_wOnHX2NCcw-TzDwCLcB/s72-c/HOK1.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/rc-shinyanga-apiga-marufuku-kufanya.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/rc-shinyanga-apiga-marufuku-kufanya.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy