REAL MADRID YATOKEA NYUMA NA KUITOA NJE YA MICHUANO YA UEFA NAPOLI

Real Madrid imetokea kufungwa goli moja nyuma dhidi ya Napoli katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora na kutinga robo fainali kwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-1.

Napoli iliyotawala sehemu ya nusu ya kwanza ya mchezo huo ilipata goli la kuongoza katika dakika ya 24 wakati Dries Mertens alipoifungia Napoli goli la kwanza baada ya beki ya Real kupoteana.

Hata hivyo Kapteni Sergio Ramos alisawazisha goli hilo na kisha kusababisha lingine la kujifunga la Mertens na kisha baadaye Alvaro Morata alifunga kwa kufuata shuti la Cristiano Ronaldo na kukamilisha ushindi.
                                           Dries Mertens akishangilia baada ya kufunga goli 

          Kapteni wa Real Madrid Sergio Ramos akiupiga kichwa mpira uliosawazisha goli
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post