ROUHANI : ECO ITAKUWA UNGUO WA MAELEWANO YA MASHARIKI NA MAGHARIBI

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, mataifa yanayostawi kiuchumi barani Asia yataufanya uchumi wa dunia utoke Magharibi na kuelekea Mashariki na mabadiliko hayo yatapelekea bara hilo kuwa mbele katika karne ya 21.
Rais Rouhani amesema hayo leo katika kikao cha 13 cha viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ECO mjini Islamabad Pakistan na kuongeza kuwa, moyo wa uchumi wa dunia kuanzia nusu karne ya hivi sasa (2017) na kuendelea utakuwa ni bara la Asia na tathmini za kiuchumi zinaonesha kuwa, jumuiya ya ECO itakuwa na nafasi na umuhimu mkubwa zaidi katika eneo hili kwenye siku za mbele.
Amesema, bara la Asia lina njia kuu za kiistratijia duniani, linapakana na bahari kuu tano na lina utajiri mkubwa wa nishati dunia na jambo hilo limeipa jumuiya ya ECO umuhimu mkubwa wa kijeopolitiki kwani linaifanya njia ya biashara ya barani Ulaya kuelekea barani Asia kuwa fupi zaidi.
Amesema, Iran ni moja ya waanzilishi wa jumuiya ya ECO, inapakana na nchi sita wanachama wa jumuiya hiyo, ina utajiri mkubwa wa mafuta na gesi duniani, ni kituo muhimu cha mawasiliano ya kieneo na ina uwezo mkubwa wa kielimu hasa wa teknolojia za kisasa, hivyo iko tayari kutoa mchango unaohitajika kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya wanachama wa jumuiya hiyo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post