SAKATA LA MCHANGA WA MADINI LASHIKA KASI, WAZIRI MKUU ATINGA MGODINI SHINYANGA

SHARE:

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuchukua sampul...

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuchukua sampuli za mchanga katika makontena mbalimbali kwa lengo la kwenda kuyapima kwa wataalamu wa madini ili kubaini kiasi cha dhahabu kilichomo.
Amesema wanataka kuona mchanga unaosafirishwa na mwekezaji huyo unakiasi gani cha dhahabu, pia Serikali inataka kufahamu kama kodi inayolipwa ni sahihi.” Hata hivyo tayari Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli alishatoa tangazo la kuzuia usafirishaji wa michanga kwenda nje ya nchi,”.
Waziri Mkuu alitembelea mgodi huo jana jioni (Jumatatu, Machi 27, 2017) na kuchukua sampuli za mchanga kwa lengo la kuondoa mashaka juu ya kinachosafirishwa. Sampuli hizo amezichukuwa kwenye makontena yaliyofungwa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.
“Tumeamua kuchukua sampuli za mchanga ambao mwekezaj anasema wanaupeleka nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kutenganisha madini ya dhahabu na shaba. Hata hivyo nimemuhoji kwa nini mitambo hiyo isiletwe nchini ili kila kitu kifanyike hapahapa,”
Waziri Mkuu amesema sera ya uwekezaji inasema mtambo huo unatakiwa uwepo nchini ili kila hatua ya uchenjuaji ifanyike hapa hapa, hivyo tunataka kujiridhisha na mwenendo wa mwekezaji na mapato tunayoyapata kama yanastahili.
Aliongeza kwamba “Hili lipo miongoni mwa masharti ya uwekezaji kwenye sekta ya madini nchini kwamba mitambo hiyo ije kujengwa hapa nchini na itaongeza fursa ya ajira na kukuza sekta nyingine ikiwemo ya kilimo,”.
Wakati huohuo Waziri Mkuu amewataka Watanzania kuwa nasubira wakati Serikali ikiendelea na zoezi la kuchunguza athari zitokanazo na kusafirisha mchanga wa madini nje ya nchi. Pia amewatoa wasiwasi wafanyakazi katika migodi na wamiliki kutowapunguza na badala yake waache waendelee na majukumu yao.
Kwa upande wake Meneja Uendelezaji wa mgodi huo Bw. George Mkanza alisema mgodi huo ulionzishwa mwaka 2009 umeajiri watumishi 720 pamoja na vibarua 500.
Alisema kwa siku wanachenjua makontena matatu hadi sita ambapo katika kila kontena moja wanapata kilo tatu za madini ya dhahabu na tani nne za madini ya shaba.
Bw. Mkanza alisema wanazalisha asilimia 50 ya madini ya dhahabu na asilimia 50 ya dhahabu iko kwenye mchanga na inakuwa imechanganyika na madini ya shaba ambayo ndiyo unaosafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutenganishwa.
“Hapa Buzwagi tuna makontena 179, makontena mengine 152 yako Dar es Salaam kwenye bandari kavu ya Nazam na 21 yako bandarini. Kila siku tunapoendelea kuzalisha tunakuwa na makontena manne hadi sita. Ndugu zetu wa Bulyanhulu nao wanamakontena 108 yako mgodini na 104 yako Nazam Cargo Dar es Salaam,” alisema.
IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
S. L. P. 980, 
DODOMA. JUMANNE, MACHI 28, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia Sampuli ya Mchanga wenye Dhahabu unao safirishwa Nnje ya Nchi na Mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama Mkoani Shinyanga Waziri Mkuu Alifika katika Mgodi huo 27march2017 kuangalia na kuchukua Sampuli ya Mchanga ili Serekali Ikaupime katika Maabara za Serekali. Picha na PMO
Mtaalamu wa Madini akiweka Sampuli ya Mchanga katika Mfuko kutoka katika baadhi ya Makontena na kumkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nakuondoka nao kwa ajili ya kuupeleka katika Maabara ya Serekali inayo shugulika na Upimaji wa Madini Wziri Mkuu alifanya ziara katika mgodi wa Buzwagi 27March2017 kwalengo ya kujionea aina ya Mchanga unao safirishwa nnje ya Nnchi na Baadhi ya Migodi inayo Chimba Dhahabu hapa Nchini .Picha na PMO
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro katika Uwanja wa Ndege wa Mgodi wa Buzwagi 27March2017 katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telaki Viongozi hao walifika kumpokea Waziri Mkuu alipofika kuangalia shughuli za Mgodi wa Buzwagi uliopo wilaya Kahama Mkoa wa Shinyanga. Picha na PMO
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa afanya ziara katika Mgodi wa Buzwagi 27 March 2017 kwa ajili ya kuangalia Mchanga uliowekwa katika Makontena kwa ajili yakusafirishwa nnje ya nchi katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telaki, na kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Stewart Hamilton. Picha na PMO

Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi walifika kumpokea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika Mgodi . Picha zote na PMO

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: SAKATA LA MCHANGA WA MADINI LASHIKA KASI, WAZIRI MKUU ATINGA MGODINI SHINYANGA
SAKATA LA MCHANGA WA MADINI LASHIKA KASI, WAZIRI MKUU ATINGA MGODINI SHINYANGA
https://3.bp.blogspot.com/-T0qgWSpDMJg/WNtRN0axDdI/AAAAAAAAY0s/e3VqptazSlAtV5empXi_4ZmYcWlwQb6CQCLcB/s1600/xRG1A0204-640x375.jpg.pagespeed.ic.HOAyQ3h0W3.webp
https://3.bp.blogspot.com/-T0qgWSpDMJg/WNtRN0axDdI/AAAAAAAAY0s/e3VqptazSlAtV5empXi_4ZmYcWlwQb6CQCLcB/s72-c/xRG1A0204-640x375.jpg.pagespeed.ic.HOAyQ3h0W3.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/sakata-la-mchanga-wa-madini-lashika.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/sakata-la-mchanga-wa-madini-lashika.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy