SAMATTA APIGA BAO MBILI STARS IKISHINDA BAO MBILI

TAIFA STARS imerejesha tabasamu kwa mara nyingine kwenye sura za mashabiki wake baada ya jioni ya jana kuifunga Botswana kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

Mabao yote mawili ya mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki wengi kiasi yametiwa kimiani na nahodha,Mbwana Ally Samatta katika dakika ya 3 na 87.

Samatta alifunga bao la kwanza baada ya kuwaponyoka mabeki wa Botswana kisha akafunga bao la pili kwa mkwaju wa faulo uliopatikana baada ya yeye wenyewe kufanyiwa madhambi.

Taifa Stars itarejea tena dimbani katikati ya wiki ijayo kucheza mchezo wake wa pili wa kirafiki kwa kuvaana na Burundi.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post