SERGIO AGUERO AIREJESHA MANCHESTER CITY KATIKA NAFASI YA TATU

Sergio Aguero amefunga goli la tano katika michezo mitatu ya hivi karibuni aliyoichezea Manchester City na kuirejesha katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kwa kuifunga Sunderland magoli 2-0.

Sunderland ilianza kwa kujilinda vyema kabla ya Manchester City kuwazidi maarifa pale Aguero alipoutumbukiza kimiani mpira wa krosi ya chini iliyopigwa na Raheem Sterling.

Wageni Manchester City walicharuka tena pale David Silva alimpomlisha pande winga kinda Mjerumani Leroy Sane na kutumbukiza goli la pili.
                                       Sergio Aguero akifunga goli la kwanza la Manchester City


                                          Leroy Sane akitumbukiza goli la pili la Manchester City
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post