SERIKALI KUANZA KUUZA HUDUMA ZITOLEWAZO NA WIZARA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nuru Millao amewataka Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kuuza huduma zitolewazo na Wizara au Taasisi husika kwa lengo la kutekeleza shughuli za Serikali.
Ameyasema hayo mjini Dodoma katika Ukumbi wa Hazina ndogo wakati wa Kikao Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kilicholenga kuwajengea uwezo Maafisa  Mawasiliano Serikalini.
“Katika kikao hiki tutapata nafasi ya kujadiliana namna bora ya kuboresha mawasiliano katika maeneo yetu ya kazi, kuisemea Serikali, kuitendea haki Serikali katika kuwasilisha taarifa mbalimbali za Serikali” amesema, Millao.
Kwa upande wake Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dotto Paul amesema kuwa wajibu mkuu wa Maafisa Mawasiliano Serikalini ni Kufuatilia kwa ukaribu nini kimeripotiwa kwenye vyombo vya habari kwa lengo la kuwa tayari kujibu au kufuatilia habari zinazohusu Serikali.
Hata hivyo, Theofil Makunga kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) akiwasilisha mada kuhusu mtazamo wa Wahariri kwa Maafisa Mawasiliano wa Serikali, amewataka Maafisa Mawasiliano kuhakikisha wanasimamia idara zao ipasavyo kwa kutoa  taarifa sahihi kwani vyombo vya habari vinawategemea kwa kiwango kikubwa
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post