SHAMSA FORD AAMUA KUMSOMEA DUA ALIYEHACK INSTAGRAM ACCOUNT YAKE!

SIku chache zilizopita tulizinyaka taarifa za mrembo wa Bongo Movie Shamsa Ford kudukuliwa account yake ya mtandao wa instagram iliyokuwa inazaidi ya followers million 2 na laki 1. Huku hacker wa account hiyo akijitapa kwa kufanya mambo ambayo ni kinyume kama kutukana watu na vitu kama hivyo.
Shamsa Ford alionyesha nia ya kuweka subira katika jambo hilo huku akiamini huenda ataipata tena account hiyo bila mafanikio, na hatimaye ameamua kufanya maamuzi ya mwisho na amedai litakalo kuwa na liwe.
Shamsa Ford amefunguka kuwa anataka kumsomea hacker huyo dua (Ahlal Badir), kwakuwa yeye ni mtoto wa kiislam, hiyo ndio njia pekee iliyobaki ya kumshtakia Mwenyezi Mungu ikiwa inafahamika fika dua hiyo huwa inamdhuru mtu aliyetenda uovu.
Bila kupoteza time, bonyeza play kwenye video hii hapa chini uweze kumsikiliza Shamsa Ford akifunguka mwenyewe kwa kinywa chake kuhusiana na issue hiyo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post