TAARIFA MPYA KUHUSU ALIYEMTISHIA NAPE NNAUYE KWA BASTOLA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba amesema mtu aliyemtishia kwa bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye si askari wa Jeshi la Polisi.
Waziri Nchemba aliyesema hayo jana alpokuwa akifungua mkutano wa kazi wa mwaka wa maofisa waandamizi wa polisi, makamanda wa mikoa na wakuu wa vikosi wa Jeshi la Polisi ambao unafanyika mjini Dodoma.
Alieleza kuwa mtu huyo aliyemtishia Mbunge Nape Nnauye mbele ya umati wa waandishi wa habari tayari ameshakamatwa na hatua kali dhidi yake zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.
“Ameshapatikana na atashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za ulinzi na usalama ambazo zimekuwa zikifanyika ndani, lakini hazitangazwi,” alisema Waziri Nchemba
Licha ya Waziri Mwigulu kusema kuwa mtuhumiwa huyo si Polisi, alikataa kuelezea kwa undani kuwa anatokea chombo gani cha ulinzi hapa nchini au jina lake kwa kile alichosema kuwa ni kwa sababu ya usalama wake.
Tukio la Nape Nnauye kutishiwa kwa kutumia bastola lilitokea juma lililopita wakati alipokwenda katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam ili kuzungumza na waandishi wa habari ikiwa ni baada ya Rais Dkt Magufuli kutengua uteuzi wake.
Mtu huyo alikwenda kwenye gari la Nape mara baada ya kushuka katika viunga vya hoteli hiyo huku akimuamrisha arudi kwenye gari na kuondoka. Lakini Nape alimtaka mtu huyo kutotumia nguvu huku akitaka ajitambulishe yeye ni nani. Kufuatia ubishi huo, mtuhumiwa huyo alitoa bastola na kumtishia Nape ili akubali kurudi kwenye gari.
Baada ya tukio hilo, Waziri Nchemba alimuagiza IGP Ernest Mangu kufanya uchaguzi kuhusu tukio hilo na kumkamata muhusika kwani Nape Nnauye si mhalifu na hana historia ya uhalifu hivyo kutolewa bastola hadharini si sahihi.
Mh Nape sio jambazi, hana record za uhalifu. Kitendo cha kutolewa bastola si cha Kitanzania na si cha kiaskari. Nimemuagiza IGP achukue hatua.”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post