TAMTHILIYA YA KICHINA YA 'MFALME KIMA' ILIYOTAFSIRIWA KISWAHILI YAZINDULIWA NCHINI

SHARE:

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante ole Gabriel (wa nne kutoka kushoto) na Naibu Waziri wa Masuala...

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante ole Gabriel (wa nne kutoka kushoto) na Naibu Waziri wa Masuala ya Utangazaji, Filamu na Habari wa China, Tong Gong (katikati), wakikata utepe kuzindua maonyesho ya kwanza ya tamthiliya ya China ya ‘Mfalme Kima’ iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kushoto ni Jiang Almin, ambaye ni Mkurgenzi wa Radio China Kimataifa, wa pili kutoka kulia ni Suzan Mungy (Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma na Matukio wa Shirika la Utangazaji Tanzania – TBC) na wa nne kulia ni Ma Li (Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Kimataifa wa China).
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante ole Gabriel, akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya tamthiliya ya China ya ‘Mfalme Kima’ iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.
Ma Li, Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Kimataifa wa China, akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo hii jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa StarTimes, Guo Zingi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamthiliya ya ‘Mfalme Kima’ ambayo ni ya Kichina iliyotafsiriwa kwa Kiswahili.
Suzana Mungy, Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma na Matukio wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamthiliya ya Kichina ya ‘Mfalme Kima’ iliyotafsiriwa Kiswahili. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurgenzi wa Radio China Kimataifa, Jiang Almin, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Meza kuu ya wageni wa heshima katika uzinduzi huo.
 Akinadada wa StarTimes wakiwa wamejiandaa kabla ya kukatwa kwa utepe kuashiria uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya China ya Mfalme Kima iliyotafsiriwa kwa Lugha ya Kiswahili.
Wageni waalikwa wakifuatilia mambo yaliyokuwa yakiendelea.
 Wasanii wakitumbuiza kwenye uzinduzi huo.
                                                                                 Wageni mbalimbali wakifuatilia.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa StarTimes, wasanii wa wageni wa heshima. 

                                                                                                         Na Dotto Mwaibale 

SERIKALI ya China kupitia Wizara ya Utamaduni ya nchi hiyo imeombwa kutangaza filamu za Tanzania nchini humo ili kuutangaza utamaduni wa Watanzania. 

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam leo hii na Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma na Matukio wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Suzana Mungy, wakati akitoa hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBC katika hafla ya uzinduzi wa maonesho ya kwanza ya Tamthiliya ya China ya (Mfalme Kima) ya lugha ya Kiswahili uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam leo. 

“Ni vema sasa na wenzetu wa China wakawa wanaonesha filamu zetu huko kwao kwa lugha ya Kichina ili kusaidia kutangaza utamaduni wetu,” alisema Mungy. 

Mungy alisema Wachina wamekuwa wakionesha filamu zao hapa nchini ambazo zimeingizwa sauti kwa lugha ya Kiswahili na Watanzania hivyo ili kupanua wigo wa mahusiano katika tasnia hiyo ni vema pande zote mbili zishirikiane kuandaa tamthiliya ya pamoja ya lugha ya Kiswahili. 

Mkurugenzi Mtendaji wa StarTimes, Guo Zingi, alisema kwamba kampuni yake imejizolea mashabiki wengi nchini Tanzania kutokana na kuonesha filamu na tamthiliya nyingi za Kichina zilizotafsiriwa Kiswahili, lugha ambayo inaeleweka. 

Alitolea mfano tamthiliya ya Maudodo, kama mojawapo ya tamthiliya hizo ambayo ilijizolea umaarufu kwa watu wa rika zote nchini Tanzania. 

Aidha, amekiri kwamba, kwa sasa ziko tamthiliya na filamu nyingi za Kichina zinazotazamwa nchini Tanzania ambazo zimetafsiriwa Kiswahili. 

Alisema mapema mwaka 2016 kampuni hiyo ilifanya mashindano ya kuwapata vijana 10 wa Kitanzania waliopelekwa China kwa lengo la kwenda kuingiza sauti za Kiswahili katika filamu na tamthiliya mbalimbali za Kichina, hatua ambayo imesaidia kuzifanya tamthiliya hizo zipendwe na kukubalika nchini Tanzania. 

Naibu Waziri wa Masuala ya Utangazaji, Filamu na Habari wa China, Tong Gong, alisema uhusiano huo baina ya Tanzania na China utaendelea kudumishwa katika masuala ya utamaduni kama iliyo katika maeneo mengine maendeleo. 

Kupitia tamthiliya mbalimbali, watakuwa wakibadilisha utamaduni baina ya nchi hizo mbili. 

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante ole Gabriel, alisema Tanzania na China wataendelea kushirikiana na kudumisha uhusiano ulioasisiwa na waasisi wa mataifa hayo – Mwalimu Julius Nyerere na Mao Tsetung. 

“Kwa kuwa wenzetu China mko juu katika teknolojia ya utangazaji na mawasiliano, ninawaomba muangalie namna ya kuisaidia Tanzania katika tasnia ya sanaa na utamaduni ili na wasanii wetu nao kazi zao ziweze kupata masoko huko,” alisema Profesa Ole Gabriel. 

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: TAMTHILIYA YA KICHINA YA 'MFALME KIMA' ILIYOTAFSIRIWA KISWAHILI YAZINDULIWA NCHINI
TAMTHILIYA YA KICHINA YA 'MFALME KIMA' ILIYOTAFSIRIWA KISWAHILI YAZINDULIWA NCHINI
https://3.bp.blogspot.com/-rHKqyLZZ_X8/WNPKyT6EqtI/AAAAAAAAYhs/SJGaxCTtW_Ujp0F-gv1jCTgmfQV4XJV8wCLcB/s1600/KIMAO.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-rHKqyLZZ_X8/WNPKyT6EqtI/AAAAAAAAYhs/SJGaxCTtW_Ujp0F-gv1jCTgmfQV4XJV8wCLcB/s72-c/KIMAO.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/tamthiliya-ya-kichina-ya-mfalme-kima.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/tamthiliya-ya-kichina-ya-mfalme-kima.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy