THIBAUT COURTOIS AIGWAYA REAL MADRID

Mlinda mlango wa Chelsea Thibaut Courtois ameonyesha dhamira ya kutaka kubaki na klabu hiyo kwa kuutaka uongozi kuharakisha suala la kumsainisha mkataba mpya.
Dhamira hiyo ya Courtois inaanza kufuta ndoto za mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid za kutaka kumsajili mlinda mlango huyo kutoka nchini Ubelgiji mwishoni mwa msimu huu, hivyo huenda wakahamishia mpango huo kwa mlinda mlango mwingine.
Courtois kwa kipindi cha miezi kadhaa amekua akihusishwa na mpango wa kusajiliwa na Real Madrid ambao tayari wameshatangaza wataachana na mlinda mlango wao wa sasa Keylor Navas.
Courtois mwenye umri wa miaka 24, bado ana mkataba na klabu ya Chelsea hadi mwaka 2019, na imeanza kuhisiwa huenda akasaini mkataba wa muda mrefu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post