TIMU YA LIVERPOOL YAISHINDILIA MAGOLI MATATU ARSENAL

Liverpool imepata ushindi muhimu katika kuwania nafasi nne za juu za Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuifunga Arsenal kwa magoli 3-1 katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Anfield.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, alifanya kosa la kumuanzisha benchi Alexis Sanchez ambaye ni kinara wao wa kupachika magoli aliyekwisha funga magoli 17 katika mchezo ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Roberto Firmino alifunga goli la kwanza na kisha Sadio Mane akafunga goli tamu la pili kabla ya mapumziko. Sanchez alitokea benchi katika kipindi cha pili na kumtengenezea goli Danny Welbeck, kabla ya Georginio Wijnaldum kufunga goli la tatu dakika za majeruhi.
                           Danny Welbeck akifunga goli pekee la Arsenal katika mchezo huo
                                               Msenegal Sadio Mane akifunga goli la pili la Liverpool 
                       Georginio Wijnaldum akifunga goli la tatu katika dakika za mwisho 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post