TIWA SAVAGE ANYOOSHA MAELEZO JUU YA MADAI HAYA NDANI YA LABEL YA ROC NATION YA JAY Z

limekuwa suala zito kwa wasanii wengi wanaosign na label kubwa za Marekani mara nyingi huishia kupotea kwenye game, na Tiwa Savage ni miongoni mwa wasanii waliohofiwa kutokewa kwa jambo hilo baada ya kusign mkataba na Roc Nation label ya Jay Z.
Kwa mujibu wa ripoti ya Urban View ya Nigeria, mwaka jana, Jay Z alishawishiwa na uwezo wa Tiwa na alikubali kumsign mnamo May 24 mwaka jana. Ilidaiwa kuwa deal lilisimamiwa na wawakilishi wa Roc Nation, Briant Biggs na Shawn Pecas. Tiwa Savage ndiye msanii wa kwanza kutoka Nigeria kusainishwa kwenye label hiyo na alijiunga na Rihanna, Big Sean, DJ Khaled na wengine.
Jay Z, Tiwa Savage & Don Jazzy
Katika Interview ya hivi karibuni na NotJustOK TV ya Nigeria. Tiwa alifunguka vitu vingi vya maisha yake ya sasa ikiwemo pia maisha yake ya kimuziki toka ajiunge na Roc Nation.
Moja ya vitu alivyoviweka sawa ni pamoja na kunyoosha maelezo juu ya madai yaliyowahi kutolewa na wadau baada ya kujiunga na label hiyo kubwa kutoka Marekani, madai hayo yalisema “Roc Nation inamlazimisha kubadilisha aina ya muziki anaoufanya” ambapo alisema..

“Ninachokipenda kuhusu kukutana na kukaa na Jay Z ni alituambia mimi na Jazzy kuwa hataki nibadilike, alinizuia kabisa. Alisema kwa msisitizo kuwa kilichomvutia kuhusu mimi na brand yangu ni kile nilichokuwa nakifanya”
Mbali na hilo, Tiwa Savage pia alichukua time na kuweka sawa kuwa bado yupo Mavin Records na Don Jazzy
“Nimesigniwa Roc Nation, nina mkataba wa kuwa- managed huko lakini label niliyopo ambayo ni familia yangu bado ni Mavin Records
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post