TRUMP AKIRI KUONGEZEKA KWA JINAI MAREKANI

Rais Donald Trump wa Marekani amekiri kuwa uhalifu, machafuko, jinai na mashambulizi ya silaha yameongezeka nchini humo.
Shirika la habari la IRIB limemnukuu Donald Trump akisema hayo kwenye hotuba yake kwa Baraza la Congress la Marekani na kutaka hatua kali zichukuliwe za kukabiliana na uhalifu wa kutumia silaha, jinai na umaskini nchini humo.
Aidha ameelezea wasiwasi wake kutokana na kuongezeka vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha na mauaji mwaka 2015 kiasi kwamba mwaka huo kiwango cha mauaji nchini Marekani kilikuwa kikubwa zaidi katika kipindi cha nusu karne nzima.
Mwaka jana wa 2016, zaidi ya watu elfu nne walipigwa risasi katika mji wa Chicago pekee bali kiwango cha mauaji mjini humo kimeongezeka zaidi mwaka huu.
Rais wa Marekani amesema, kila mtoto wa nchi hiyo anapaswa kuishi katika mazingira salama ya kijamii.
Licha ya makundi ya kutetea haki za raia nchini Marekani kutaka kupigwa marufuku kuuzwa silaha kiholela nchini humo, lakini lobi zenye nguvu za masuala ya silaha hadi hivi sasa zimeizuia Ikulu ya nchi hiyo kuweka sheria za kupiga marufuku jambo hilo.
Silaha nchini Marekani zinauzwa kama bidhaa nyingne za kawaida madukani na jambo hilo limepelekea kuenea silaha mikononi mwa watu ambao hawasiti kuzitumia kila wanapokasirishwa na jambo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post