UKUMBI WA CCM WAPEWA JINA LA RAIS DKT KIKWETE (KIKWETE HALL)

Wakati Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ukiendelea Dodoma, ukumbi wa mikutano wa chama hicho umepewa jina la Rais  na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Dkt Jakaya Kikwete.
Ukumbi huo kuanzia leo utakuwa unafahamika kama Kikwete Hall (Ukumbi wa Kikwete) baada ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum kuridhia pendekezi hizo.
Pendekezo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt Magufuli ambapo alisema kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Rais Kikwete katika ngazi ya chama, basi kwa heshima waupe jina lake ukumbi huo. Wajumbe wote waliridhia mapendekezo hayo.
“Leo tumekaa katika ukumbi huu mzuri, kuna watu wamefanya kazi na miongoni mwao atakuwa ni Mzee wetu Jakaya Kikwete (Rais Mstaafu wa awamu ya nne). Mtakumbuka kabla ya hapa tulikuwa tukikaa kule yanatolewa magunia tunakaa, Hivyo kama mtanikubalia naomba ukumbi huu tuuite jina la Kikwete Hal”amesema.
WhatsApp Image 2017-03-12 at 1.52.04 PMKikwete Hall
Akizungumza, Rais Jakaya Kikwete alisema kuwa kuwa anashukuru sana kwa heshima hiyo aliyopewa licha ya kuwa ni maamuzi yaliyofanywa bila kumshirikisha na pengine kama angeshirikishwa angechukua muda kukubali.
Lakini pia, Rais Kikwete amemuomba Mwenyekiti Dkt Magufuli kumpatia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana heshima kama aliyompatia yeye kwani amefanya kazi kubwa sana ya kuhakikisha kuwa chama kinaendelea kuwa imara.
Tayari mabadiliko ndani ya CCM yamefanywa na Mkutano Mkuu, ambapo kwa kauli moja wameyaridhia na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt Magufuli ameahirisha mkutano huo hadi wakati mwingine.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post