‘UNGA’ UNAVYOELEKEA KUANGAMIZA MAISHA, KIPAJI CHA CHRIS BROWN

LOS ANGELES, Marekani
MWANAMUZIKI Chris Brown ni miongoni mwa mastaa waliojizolea umaarufu mkubwa kutokana na maisha yao ya kila siku kutawaliwa na vituko.
Kwa sasa supastaa huyo anatajwa kuwa na matatizo ya akili tangu alipotemwa na meneja wake. Matatizo hayo yanatajwa kuchangiwa na utumizi wa dawa za kulevya.
Meneja Mike Guirguis aliachana na Chris mwaka jana huku akidai kudundwa na mwimbaji huyo na kulazimika kulazwa hospitali.
Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la New York Daily News, Mike G, alidai Chris alimwalika nyumbani kwake na ghafla alianza kumshambulia kwa ngumi nzito.
Itakumbukwa hata alipomshambulia kwa makonde aliyekuwa mpenzi wake, Rihanna, mwaka 2009, Chris alitajwa kuwa alikuwa ametumia dawa za kulevya.
Siku chache baada ya tukio hilo, Chris alikiri kuhudhuria ‘rehab’. Pia, ilisemekana kuwa kuachana na Karrueche Tran kulitokana na sababu hiyo.
Lakini sasa, baada ya Mike G kujiweka kando na shughuli zote zinazomhusu Chris, imeelezwa kuwa hali ni mbaya kwa mkali huyo kwani ameongeza ‘dozi’ ya dawa za kulevya.
Taarifa zimedai Chris hayuko sawa na amekuwa akitumia dawa za kulevya  kwa kiasi kikubwa, jambo linalotishia hatima ya maisha na kazi yake ya muziki.
Mmoja kati ya walinzi wake wa karibu alisema: “Baada ya kumfanyia vile Mike G, kila kitu kiliharibika.”
“Hatukuwa na meneja wa kutuambia cha kufanya na wapi tunaelekea. (Chris) akikasirika, anaweza kuwaambia watu walale kwenye gari (badala ya hotelini). Alikuwa akiwatisha watu na polisi. Alikuwa akijiita shetani.”
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari za burudani, idadi kubwa ya wafanyakazi wake wameshamkimbia Chris.
Miongoni mwao ni aliyekuwa msimamizi wa ziara za kimuziki za staa huyo, Nancy Ghosh, ambaye alidai Chris alitishia kumpiga.
Mtaalamu wake wa matangazo, Nicole Perna, naye alikimbia kibarua kwa madai kuwa bosi wake huyo alimkashifu kwa madai kuwa alishindwa kutangaza kampuni yake ya mavazi ya Black Pyramid.
Lakini pia, hata marafiki wa karibu wa Chris wamekuwa wakiogopa kumsogelea mshikaji wao huyo kutokana na hali yake ya sasa.
“Huwezi kuzungumza na ‘mteja’, mtu ambaye hayuko sawa. Haingii akilini,” alisema mmoja wa marafiki zake.
“Ni jambo unalotakiwa kulifanyia kazi. Unatakiwa kubadili mfumo wako wa maisha. Hafanyi kile kinachopaswa kufanyika ili kurejea katika uzima, hivyo hawezi kuwa sawa.”
Kwa sasa watu pekee waliobaki karibu na Chris wanatajwa kuwa ni ndugu zake wa damu akiwamo mama yake mzazi.
Kwa wasiomfahamu, jina lake halisi ni Christopher Maurice “Chris” Brown na alizaliwa Mei 5, 1989. Ngoma yake ya kwanza ni ‘Run It!’ ambayo ilishika nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post