UTEUZI WA MAMA SALMA KIKWETE WASABABISHA MGAWANYIKO MKUBWA

Siku moja baada ya Rais Dkt Magufuli kumteua Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watu wa kada mbalimbali wamejitokeza na kutoa maoni yao kuhusu uteuzi huo kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Baadhi ya watu waliotoa maoni yao kuhusu uteuzi wa Salma Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete wamepongeza hatua hiyo huku wengine wakisema kuwa ameshushwa cheo kutoka ‘First Lady’ hadi kuwa Mbunge.
Akitoa maoni yake, Mratibu wa Taifa wa Taasisi ya Wanawake ya Ulingo, Dkt Ave Maria Semakafu alisema uteuzi huo ni bora kwani rais ameona anafaa hivyo ametimiza wajibu wake wa kikatiba.
Aidha, aliongeza kuwa Salma Kikwete ni mmoja kati ya wanawake wenye mchango mkubwa kwenye siasa za Tanzania huku akiwa mzuri kwenye masuala ya kufanya maamuzi. Mimi sioni tatizo la uteuzi huo, na kama unavyojua sisi tunapigania kuongeza uwiano wa wajumbe ndani ya bungeni, hivyo kwetu sisi hii ni hatua kubwa, alisema Dkt Ave.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dk. Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa uteuzi huo ni kumshusha hadhi Salma Kikwete.
Naona kama wamemshusha hadhi, yeye amefanya kazi kubwa wakati akiwa mke wa rais kwa miaka 10, nadhani huu ulikuwa wakati wake apumzike baada ya kumaliza majukumu yake. Nafasi hiyo naona angepewa mwanamke mwingine mwenye mawazo mapya na si yeye aliyepaswa kupumzika.
Akizungumzia uteuzi wa mama yake, Ridhiwani Kikwete ambaye ni Mbunge wa Chalinze amesema kuwa anaamini mama yake ni mwanamke aliyeyaanzisha mapambano na kuwasaidia wanawake wengi na watoto wa kike kupata elimu hivyo kuteuliwa kwake kuwa mbunge kutasaidia kuendeleza mapambano hata ndani ya bunge.
“Umekuwa mtetea wa haki za wanawake na usawa wa kijinsia, umewezesha wasichana kupata elimu.Wewe ni Mwanamke wa Shoka.Hongera sana kwa uteuzi.” Ameandika Ridhiwani Kikwete.
Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Susan Lyimo alisema kwa mtazamo wake uteuzi huo ni kumshusha hadhi aliyokuwa tayari amejijengea kwenye jamii.
Hiyo kwangu naona kama kushushwa cheo, naamini Rais angeweza kuteua mwanamke mwingine kutoka ndani ya chama lakini siyo yeye. Kwanza akija kule bungeni anakutana na mtoto wake, alisema Susan Lyimo
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post