VIDATO VINNE VYAMPA JEURI DALALI SIMBA

NA SALMA MPELI
MWENYEKITI wa zamani wa Simba, Hassan Dalali, amesema sasa ana vigezo vyote vya kuwania uongozi wa klabu hiyo ikiwamo elimu.
Dalali  alienguliwa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa Simba uliofanyika mwaka juzi kutokana na kutokidhi kigezo cha elimu.
Kufuatia hatua hiyo, aliamua kurejea darasani na kusoma masomo ya sekondari ambapo alihitimu kidato cha nne.
Akizungumza jijini Dar es Salam jana, Dalali alisema kwa sasa hana mpango wa kuwania uongozi katika klabu hiyo licha ya kwamba anavyo vigezo vya kufanya hivyo.
“Kwa sasa nipo vizuri, nimejipanga na nimejikamilisha, nimesoma na vyeti ninavyo, sijasema kama nimepanga kugombea uchaguzi ujao lakini elimu niliyonayo itanisaidia katika mambo mengi,” alisema Dalali ambaye kwa sasa ni maarufu kwa jina la Trump wa Simba.
Dalali alisema anaamini umoja na mshikamano ulioko katika klabu hiyo kwa sasa utaiwezesha kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post