VIDEO MAKONDA AKICHEZA MUZIKI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akizungumza na wakazi wa jijiji la Dar es alaam katika kuandishimisha mwaka mmoja tangu alipoanza kazi kama kiongozi wa mkoa huo, amepata nafasi ya kuimba pamoja na mwanamuziki Mrisho Mpoto na kuonyesha furaha yake kwa mengine aliyoyafanya.

Halfa hiyo imefanyika katika ukumbi wa Kituo cha Polisi Oysterbay ambapo Makonda amezungumzia mambo mbalimbali ambayo analenga kuyafanya anapoanza mwaka wake wa pili wa utumishi.

Miongoni mwa mengi aliyoyasema ni pamoja na kuendeleza vita dhidi ya dawa za kulevya kwa kasi zaidi, kuboresha miundombinu ya jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kuwahamisha wanaoishi mabondeni, masuala ya elimu, afya kupunguza uhalifu.

Kabla ya kumaliza hotuba yake, Makonda aliomba kucheza wimbo na Mrisho Mpoto huku akionyesha furaha yake ya kuwa mkuu wa mkoa kwa mwaka mmoja.


Makonda aliteuliwa kwenye wadhifa huo pamoja na wakuu wa mikoa mingine Machi 13 mwaka jana na waliapishwa na Rais Dkt Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam, Machi 15, 2016.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post