VIDEO: MKENYA AKAMATWA AKIINGIZA WAHAMIAJI HARAMU TANZANIA

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Agness E. Hokororo amekamata wahamiaji haramu wanne, watatu wa Ethiopia wanaodaiwa kuwa ni Wahabesh wanaotokea Adis Ababa Ethiopia na Mkenya mmoja Bi Jamila Hashim Abdi (44) akituhumiwa kuwa mfanikishaji wa kuingiza wageni hao mara kwa mara Nchini Tanzania.
Waethiopia hao ambao wote ni wanaume wamejitambulisha kwa majina yao :
  1. KAMSUR KADIR SIRIMLU (23)
  2. RAMADHAN ANGULEE ABDI (25)
  3. AWAL ROBA BUTAA (22)
Mhe. Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Mkuu wa Uhamiaji Tarakea Rombo Mr. HEMMANS KILEMBE walizifanyia kazi taarifa tulizozipata kutoka kwa raia mwema ambae jina lake linahifadhiwa. Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa kwenye gari aina ya Noah ndani ya Wilaya ya Rombo na walidai wanaelekea Moshi.
Kwa sasa watuhumiwa wanashikiliwa kituo kikuu cha Polisi Mkuu Rombo tayari kwa kupelekwa Moshi Uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria.
Mhe. Mkuu wa Wilaya anawaomba wananchi wote hususani waishio maeneo ya mpakani kuendelea kutoa taarifa sahihi mapema kwa watu wote wanaowatilia mashaka na mawakala wote wanaoshirikianana wahalifu ili kudhibiti raia wa kigeni, madawa ya kulevya na magendo.

Imetolewa na:
Abubakar D. Asenga
DAS – ROMBO
Simu: 0715:429738
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post