VIDEO: RAIS MAGUFULI ATUMIA WIMBO WA DARASSA KUHUTUBIA WANANCHI

Mwanamuziki Darassa sasa ana kila sababu ya kuamini kuwa wimbo wake wa Muziki alioutoa mwishoni mwa mwaka jana ni wimbo wake uliokubalika na kufanya vizuri zaidi.
Watu wengi wamekuwa wakiusikiliza na hata ukipigwa katika kumbi za starehe hata waliokaa uvumilivu huwashinda na kuanza kusakata ngoma hiyo. Mbali na wapenda burudani, lakini pia tumeona hata kiongozi wa dini, Mzee wa Upako akiutumia wimbo huu katika moja ya mahubiri yake kanisani.


Zamu hii ni Rais Dkt John Pombe Magufuli ambapo ametumia mashairi ya wimbo huu akiwa katika moja ya mikutano yake ya hadhara katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania.
Akihutubia wananchi, Rais Dkt Magufuli alinukuliwa akisema “Kwamba unaenda bila break, what do you expect,” huku wananchi waliokuwa wakimsikiliza kutoa shangwe kubwa na kisha akaongezea tena “Mkishaimbiwa changanya kama karanga ndio mnachanganyikiwa kabisa.”
Hapa chini ni video ya Rais Magufuli akihutubia wananchi na kutumia mashairi ya wimbo wa Darassa.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post