VIONGOZI WA MATAIFA WAUNGANA NA UINGEREZA BAADA YA SHAMBULIZI LA KIGAIDI

Viongozi wa Mataifa yaliyoathirika hivi karibuni na mashambulizi ya kigaidi wamepaza sauti zao za kuonyesha mshikamano na Uingereza kufuatia shambulizi la kigaidi karibu na majengo ya bunge lililouwa watu watano na kujeruhi 40.

Katika shambulizi hilo lililotokea jana na kutekelezwa na mshambuliaji mmoja aliyepigwa risasi na kufa, baada ya kutumia gari kuwagonga watembea kwa miguu na kuwauwa watu watatu na kisha kumchoma kisu na kumuua askari nje ya bunge.

Afisa aliyeuwawa ametambulika kuwa ni PC Keith Palmer, 48, ambaye ameoa na ana watoto. Waziri Mkuu Theresa May amesema muuaji ni mgonjwa na mtu wa hovyo.
Mtu aliyetekeleza mauaji hayo akiwa kwenye machela akipatiwa huduma ya kwanza
 Watoa huduma ya kwanza wakipambana kujaribu kuokoa uhai wa mtu aliyetekeleza shambulizi la kigaidi eneo la Westminster Uingereza
                                     Mwanaume mmoja aliyegongwa kwa gari akipatiwa msaada
                  Majeruhi mwingine aliyegongwa na gari na muuaji akipatiwa matibabu

                          Mwanamke aliyejeruhiwa kwa kugongwa na gari akipatiwa msaada
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post