WAASI 20 WA M23 WAUAWA MASHARIKI MWA DRC

Waasi wasiopungua 20 wameuawa katika mapigano yaliyozuka kwenye siku za hivi karibuni kati ya wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23 mkoani Kivu Kaskazini.
Léon Mushale, mmoja wa maafisa wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametangaza habari hiyo na kusema kuwa, mbali na kuuawa waasi hao 20, waasi wengine 25 wamejeruhiwa katika mapigano ya ana kwa ana kati yao na jeshi la serikali huko Kivu Kaskazini.
Amesema, idadi kubwa ya waasi hao wa M23 wamekimbilia Uganda na Rwanda baada ya kuzidiwa nguvu na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Viongozi wa Kongo wanazilaumu nchi jirani za Uganda na Rwanda kuwa zinawapa nguvu waasi hao na kusema kuwa, mashambulizi ya waasi wa M23 yataendelea kuhatarisha usalama wa Kongo hasa mashariki mwa nchi hiyo, madhali waasi hao wangali wana kambi zao katika nchi hizo mbili.
Ikumbukwe kuwa waasi wa M23 ni kundi la mwisho la waasi wa Kitutsi ambao duru mbalimbali za kieneo na kimataifa zinasema wanaungwa mkono na serikali za Rwanda na Uganda. Hata hivyo nchi hizo mbili zinakanusha kuwaunga mkono waasi hao.
Kwa kusaidiwa na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walifanikiwa kuwazidi nguvu waasi wa M23 mwaka 2013 na kukomesha mashambulizi ya zaidi ya miezi 18 ya waasi hao katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Kundi hilo lilitangaza rasmi kuacha uasi baada ya kuzidiwa nguvu. Hata hivyo viongozi wa Kinshasa wanasema kuwa, ni waasi 193 kati ya 500 wa M23 ndio waliorejea Kongo kutokea Uganda na 13 kati yao waliomba ukimbizi katika nchi jirani ya Rwanda.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post