WABUNGE WAWILI WA CCM WAKAMATWA DODOMA KWA KUTAKA KUVURUGA MKUTANO MKUU

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe,  Mbunge wa Geita Vijijini na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku Musukuma na aliyewahi kuwa Mbunge wa Kisarawe na Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima wamehojiwa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma na kisha kuachiwa kwa dhamana baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kupanga njama za kuvuruga mkutano mkuu wa CCM.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amethibisha kuwakamata viongozi hao ambapo wanadaiwa kuwa walipanga kuvuruga vikao vya CCM vinavyoendelea mjini Dodoma.
Wajumbe hao wa Mkutano Mkuu wa CCM inadaiwa kuwa walikuwa wakigawa fedha kwa wajumbe ili kuvuruga mkutano mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika kesho.
Aidha, Kamanda huyo amesema bado kuna wengine waliotuhumiwa ambapo msako wa kuwapata kwa ajili ya mahojiano unaendelea.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post