WAFANYABIASHARA WA ASALI WAPEWA MWEZI MMOJA KUACHA KUTUMIA CHUPA ZA KONYAGI

SHARE:

Wafanyabiashara wa asali katika wilaya ya Ikungi, mkoani Singida waliopo kando kando ya barabara kuu Singida-Dodoma, wamepewa muda wa mwe...

Wafanyabiashara wa asali katika wilaya ya Ikungi, mkoani Singida waliopo kando kando ya barabara kuu Singida-Dodoma, wamepewa muda wa mwezi mmoja kuanzia sasa, kutumia vifungashio halisi badala ya chupa za konyagi, ili kulinda afya za walaji.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturi, ametoa agizo hilo juzi wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa matumizi sahihi ya vifungashio vya asali, iliyofanyika katika kijiji cha Issuna tarafa ya Ikungi.
Alisema ufungaishaji wa asali unaofanywa na wafanyabiashara wa asali katika wilaya ya Ikaungi, sio wa kuridhisha na kwa namna moja au nyingine, unachangia kuharibika kwa asali.
“Ufungaishaji unao fanywa na wafugaji wetu wa nyuki,unachangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa soko la asali.Wafanyabiashara hawa wanaouzia asali pembezoni mwa barabara,wanafungasha asali bila kuzingatia sheria na kanuni za biashara ya mazao ya nyuki hususani asali.Nawapeni mwezi moja mbadilike katika ufungaishaji,” alisisitiza Mtaturu.
Mkuu wa wilaya hiyo, pia amewataka  wauzie asali  ndani ya jengo maalumu la kuuzia mazao ya nyuki ambalo toka limalizike kujengwa mwaka 2013, hadi sasa halijawahi kutumiwa.
Awali kaimu meneja wakala wa huduma za misitu wilaya ya Ikungi, Samson Lyimo,alisema asilimia 70 ya eneo la ardhi ya wilaya ya Ikungi ni misitu, miti, vichaka na nyanda za mbunga, ambayo ni rasilimali muhimu kwa ufugaji wa nyuki.
Hata hivyo, Lyimo, alisema ni asilimia ndogo ya eneo hilo linalotikika kwa shughuli za ufugaji nyuki.
“Ufugaji wa nyuki wilaya ya Ikungi,unafanywa na mtu mmoja mmoja na wengine wamejiunga katika vikundi na kufanya shughuli kwa pamoja. Hadi sasa tunayo vikundi 63 ambavyo vimesajili na vinajihusisha na uzalishaji wa mazao ya nyuki ambayo ni asali na nta,” alisema kaimu meneja huyo.
Lyimo alisema kuwa asali ambayo  imezalishwa kwa kuzingatia sheria na kanuni za ufugaji, ikachakatwa vizuri, ikafungaswa vizuri na kuwekewa lebo, ina soko zuri ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo, alisema kuwa ubora wa asali ya wilaya ya Ikungi, unaathiriwa na mambo mengi ikiwemo ya wafungaji kuvuna asali ambayo  haijakomaa.
“Wafungaji wengine wanachemsha asali baada ya kuivuna, wengine kuchanganya na maji,kuongezea asali na kuuzia barabarani kwenye joto kali,” alisema.
Akisisitiza, alisema baadhi ya wafanyabiashara huweka asali kwa kutumia vyombo ambavyo tayari vimeishatumika kufungashia bidhaa zingine kama pombe viuatilifu, maji na mafuta ya aina mbalimbali.
Lyimo alisema matumizi ya vifungaishia hivyo,ni kinyjme na kanuni za ufugaji nyuki ya 2005 sehemu ya III, kifungu cha 21 (4) (a-i).
Baadhi ya wajasiriamali, akiwemo Musa Mwanja na Nasson Lucas wameomba muda zaidi wa kujiandaa.
Hata hivyo,lmkurugenzi mtendaji halmashauri wilaya ya Ikungi, Rustika Turuka, anasema agizo hilo litatekelezwa ili kulinda soko na afya za walaji.
Uzalishaji wa mazao ya asali, hususani asali umekuwa ukiongezeka Wilayani Ikungi kutoka tani 3.74 mwaka 2015/16 hadi kufikia tani 4.416 mwaka 2016/17.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: WAFANYABIASHARA WA ASALI WAPEWA MWEZI MMOJA KUACHA KUTUMIA CHUPA ZA KONYAGI
WAFANYABIASHARA WA ASALI WAPEWA MWEZI MMOJA KUACHA KUTUMIA CHUPA ZA KONYAGI
https://1.bp.blogspot.com/-CsWJDKOS6So/WLwl3aJGgWI/AAAAAAAAXbM/cJ5rirsw-8kwlP7RdQza5FckmlUQgci4ACLcB/s1600/asali-750x375.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-CsWJDKOS6So/WLwl3aJGgWI/AAAAAAAAXbM/cJ5rirsw-8kwlP7RdQza5FckmlUQgci4ACLcB/s72-c/asali-750x375.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/wafanyabiashara-wa-asali-wapewa-mwezi.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/wafanyabiashara-wa-asali-wapewa-mwezi.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy