WAFANYAKAZI 45 WAKUTWA NA VYETI BANDIA MUHIMBILI

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha Tiba na Mifupa (MOI), Dkt. Othman Kiloloma amesema wapo katika mchakato wa kupunguza wafanyakazi 45 waliobainika kuwa walikuwa na vyeti bandia.
Akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyofika hospitali hapo juzi, Dr Kiloloma alisema kuwa wafanyakazi hao walibainika baada ya mchakato wa uhakiki wa vyeti kwa wafanyakazi wa taasisi hiyo.
Vilevile alisema kuwa taasisi hiyo ina upungufu mkubwa wa fedha kutokana na serikali kushindwa kutoa ruzuku ya TZS bilioni 4.8 zilizokuwa zitolewe kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Aliongeza kuwa  kutokana na tatizo hilo, kitengo hicho kimeshindwa kujiendesha kwani hutumia fedha nyingi sana kwa mwaka. Zaidi ya TZS bilioni 20.6 hutumika kwa mwaka kununulia vifaa vya tiba, na wakati huo huo wagonjwa zaidi ya 70% hutibiwa kwa msamaha.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Lawrence Museru alisema kuwa MNH iliidhinishwa kupewa TZS bilioni 4 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali lakini mpaka sasa haijapokea fedha hizo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post