WAFANYAKAZI BODI YA MAPATO KUANDALIWA KOZI 64

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) yatakayowezesha wafanyakazi wa Bodi hiyo kujengewa uwezo.
Mkataba huo umesainiwa jana, jijini Dar es Salaam na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Alphayo Kidata kwa niaba ya Chuo cha Kodi (ITA) pamoja na Kamishna Mkuu wa Bodi ya Mapato Zanzibar.
Kidata amesema kuna jumla ya kozi 64 zitafundishwa katika chuo hicho kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwaongezea maarifa wafanyakazi hao ili waweze kuimarisha utendaji wao.
“Kazi ya kukusanya mapato na kodi mbalimbali inahitaji elimu ya mara kwa mara hivyo ni mategemeo yetu kwamba baada ya mafunzo hayo wenzetu wa Bodi ya Mapato Zanzibar wataweza kuimarisha utendaji kazi wao hivyo kupanua wigo wa ukusanyaji mapato ya Serikali,”alisema Kidata.
Akifafanua, Kidata amesema kuwa makubaliano hayo ni muhimu katika kuimarisha utendaji kazi hivyo zoezi hilo litaanza mnamo mwezi Machi hadi Juni mwaka huu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post