WAHUDUMU 90 WA HOTELI, MIGAHAWA NA NYUMBA ZA KULALA WAGENI MKOANI NJOMBE KUPIGWA MSASA KWA MUDA WA SIKU TATU NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII NA MRADI WA SPANEST


Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki  (kushoto) akiteta neno na mgeni rasmi Katibu Tawala mkoa wa Njombe, Jackson Saitabau  mara alipowasili kuja kufungua mafunzo ya muda siku tatu kwa washiriki 90 katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yanayofanyika Mkoani Njombe
sp2
Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskas Mwiru  alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi, Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe kufungua  mafunzo hayo jana katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yanayofanyika Mkoani Njombe kwa muda wa siku tatu na yakiwa na jumla ya washiriki 90. Katikati ni Katibu tawala wa Mkoa wa Njombe pamoja na Mratibu wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki  (Picha na Lusungu Helela- WMU)
sp3
Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Jackson Saitabau akizungumza na jumla ya  washiriki  90 wakati alipokuwa akifungua jana mafunzo ya fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yanayofanyika Mkoani Njombe kwa muda wa siku tatu. na Wengine ni Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki  (kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskas Mwiru (kulia) 
sp4
Mkufunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii,Jesca William akiwaelezea washiriki wa mafunzo kusoma  kozi zinazotolewa na Chuo cha Taifa cha Utalii  mara baada ya mgeni rasmi kufungua mafunzo ya siku tatu katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yanayofanyika Mkoani Njombe. 
sp5
Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Jackson Saitabau  akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua  mafunzo ya  jumla  ya wahudumu 90 wa Hoteli, Migahawa na Nyumba za kulala wageni mkoani Njombe watakaopewa mafunzo ya siku tatu katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu. Mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST , lengo likiwa ni kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa katika sekta hiyo ili kukidhi mahitaji ya soko, pamoja na kukuza hadhi ya huduma za malazi zilizopo chini ya kiwango. Wengine ni Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki (kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskas Mwiru (kulia) 
sp6
Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mgeni rasmi  kufungua mafunzo ya muda siku tatu kwa washiriki 90 katika fani ya Utalii na Ukarimu
sp7sp8
Mmoja wa Washiriki wa mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na akielezea jambo kwa Mkufunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dawson Kyungai  mara baada ya Mgeni rasmi kufungua mafunzo katika fani ya ukarimu na Utalii.
………………………………………………………………………..
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Mradi wa SPANEST  imeanza jitihada za kuinua na kuendeleza Utalii kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa kuanza  kutoa mafunzo katika sekta ya ukarimu na utalii  kwa wahudumu 90  wa hoteli, migahawa na nyumba za kulala wageni ili kuwawezesha kutoa huduma zenye hadhi kwa watalii.
Kufuatia hali hiyo, wahudumu hao wameanza kupewa mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi kwa lengo likiwa  ni kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa katika sekta ya ukarimu na utalii ili kukidhi mahitaji ya soko, pamoja na kukuza hadhi ya huduma za malazi zilizopo chini ya kiwango kwa mikoa ya Nyanda za juu kusini
Hayo aliyasema jana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Jackson Saitabau  wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya ukarimu na utalii kwa jumla ya washiriki 90 yanayofanyika kwa muda wa siku tatu mkoani Njombe na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia Mradi wa SPANEST unaotekelezwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Aliongeza kuwa licha ya ukanda huo kuwa na  vivutio vingi vya utalii lakini idadi ya watalii imezidi kuwa ndogo, Hivyo mafunzo hayo watakayoyapata yatakuwa chachu katika kukuza na kuendeleza utalii kwa kutoa huduma zenye viwango kwa watalii pindi wanapokuja kutembelea vivutio vya utalii.
 Saitabau amewataka wahudumu waache  tabia ya uvivu na kufanya kazi kwa mazoea pindi wanapotoa huduma kwa watalii kwa kuwa wanaoharibu sifa ya Mkoa na kuwataka mafunzo watakayopata yawe chachu katika kukuza na kuendeleza utalii.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii, Paskas Mwiru amesema mafunzo hayo hayataishia kwa watoa huduma tu katika hoteli pia mafunzo hayo yataendeshwa kwa wamiliki wa sehemu hizo ili waweze kuwalipa malipo stahiki wafanyakazi wao wanaofanya kazi katika sehemu hizo.
Kwa Upande wa Mratibu wa Mradi wa SPANEST, Godwell Meing’ataki amesema  mafunzo hayo yanafanyika ili kuwawezesha wahudumu kuwa na ujasiri na kujiamini pale wanapotoa huduma kwa watalii.
‘’ Sisi tunaamini  tukiwapa ujuzi wahudumu hawa tutakuwa tumefungua milango ya watalii wengi zaidi kuja kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Nyanda za Juu kusini’’ alisema Meing’ataki
Hadi hivi sasa mafunzo yameshafanyika mkoani Mbeya na kwa sasa yanafanyika Njombe baada ya hapo yatafanyika  Iringa  na hatimaye mkoani   Songwe
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post