WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WAPIGWA MARUFUKU KUWAWEKA MAHABUSU MADAKTARI

Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amepiga marufuku Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwadhalilisha kwa kuwasweka mahabusu watumishi wa afya katika mikoa na wilaya zao.
Waziri wa Afya aliyasema hayo jana ambapo alieleza kwa sasa imekuwa kama mtindo kwa viongozi hao kuwasweka mahabusu watumishi wa afya jambo ambalo halisaidii kuboresha utoaji wa huduma za afya.
Waziri aliwataka viongozi kuwaripoti watumishi wa afya wanapovunja sheria au kukiuka taratibu za utoaji huduma ili wafutiwe leseni. Mtumishi wa afya akishafutiwa leseni hawezi kufanya kazi sehemu yoyote duniani, hivyo badala ya kuwaweka mahabusu tupeni taarifa tuwachukulie hatua za kinidhamu, alisema Waziri Mwalimu.
Ameongeza kuwa, tayari ameshakubaliana na Waziri wa TAMISEMI, George Simbachawene kuhusu kuwaelekeza Wakuu wa Wilaya na Mikoa mipaka yao ya kazi ili wasiingilie kazi na taratibu nje ya majukumu yao.
Agizo hili limekuja siku chache baada ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Singida Vijijini, Dk. Erick Bakuza kuandika barua ya kuacha kazi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Singida kumuweka ndani mganga huyo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post