WANAFAMILIA MBEYA WAKATAA KUMZIKA NDUGU ALIYEFARIKI SUMBAWANGA

Familia ya marehemu Cleva Mlawizi (32), yenye makazi katika kijiji cha Ikolomela, wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe, imegoma kuuzika mwili wa ndugu yao huyo kwa madai kuwepo kwa utata katika kifo chake.

Mwanamke huyo aliyekuwa akiishi Sumbawanga na mumewe alifariki usiku wa Machi 15. Mume wa marehemu alieleza kuwa baada ya chakula cha usiku alimuaga mkewe na kwenda kuangalia mpira kupitia runinga, lakini aliporudi alimkuta mkewe huyo akiwa amefariki tayari.
Ripoti ya daktari aliyefanyia uchunguzi maiti hiyo ilisema kuwa sababu ya kifo cha marehemu ilikuwa ni njaa.

Lakini msemaji wa familia alisema kuwa, baada ya mwili kusafirishwa kupelekwa Ikolomela, walikuta maiti ikiwa imevimba na inatokwa na damu kiashiria kuwa marehemu alipigwa na kitu kizito kichwani kabla ya kukutwa na umauti.

Kamanda wa Poilisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange, alithibitisha kupokea malalamiko ya wanafamilia hao na kusema kwamba, baada ya kufika kituoni, polisi waliwaeleza kuwa kama hawakuridhishwa na maelezo ya uchunguzi wa daktari wa awali basi waupeleke mwili huo katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya ili ufanyiwe uchunguzi wa kina.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post