WATAKAOHUJUMU MASHINE MANDARINI WATIMULIWE

Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuwatimua kazi watumishi watakaohujumu mashine za kukagulia mizigo bandarini (scanner) ili kuzuia upotevu wa mapato.
Mashine hizo za ukaguzi zilizotolewa na serikali ya China,zimegharimu Sh20.2 bilioni.
Akizungumza leo  wakati wa uzinduzi wa mashine tatu za kukagulia mizigo katika makontena, Mbarawa alisema kama wafanyakazi hawatakuwa waaminifu uwepo wa mashine hizo hautakuwa na maana.
‘‘Leo tumezindua mashine hizi za kisasa za kukagulia mizigo kwenye makontena lakini kama watumishi wetu hawatakuwa waaminifu hazitatusaidia,’’alisema na kuongeza :
‘‘Mkurugenzi Mkuu wasimamie kwa karibu watalaam watakaokuwa wanazisimamia ‘scanner’ ili zifanye kazi iliyokusudiwa, wakikosa uaminifu waondolewe.’’ alisema.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post