WATANZANIA WAASWA KUBADILIKA LA SIVYO WAKENYA NA WAGANDA WATAENDELEA KUAJIRIWA KATIKA HOTELI ZETU

SHARE:

Mkuu wa Mkoa wa  Njombe, Ole Sendeka  akizungumza na jumla ya  wahitimu 90 wakati alipokuwa akifunga jana mafunzo katika fani ya Utalii n...

Mkuu wa Mkoa wa  Njombe, Ole Sendeka  akizungumza na jumla ya  wahitimu 90 wakati alipokuwa akifunga jana mafunzo katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na Mradi wa  SPANEST yaliyofanyika Mkoani Njombe kwa muda wa siku tatu. na Wengine ni  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Njombe, Joseph Choya (kulia) Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskasi Mwiru (kushoto)
 ZETE 1
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ole Sendeka  akiwa kwenye picha ya pamoja na  baadhi ya viongozi na  Maofisa  kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Mradi wa SPANEST na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe  mara baada ya kufunga  mafunzo ya muda wa siku tatu kwa  jumla  ya wahitimu  90 katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na Mradi wa SPANEST.
ZETE 2
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ole Sendeka akikabidhi cheti kwa Mhitimu wa mafunzo katika fani ya ukarimu na utalii wakati alipokuwa akifunga mafunzo hayo jana yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na Mradi wa  SPANEST yaliyofanyika Mkoani Njombe. 
 ZETE 3

Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskasi Mwiru  alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa  mkoa wa Njombe kufunga  mafunzo hayo katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika jana Mkoani Njombe kwa muda wa siku tatu na yakiwa na jumla ya washiriki 90.
ZETE 4
Mkufunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Dawson Kyungai akiwaelekeza Washiriki 90 wa Mafunzo ya Ukarimu na Utalii namna ya kumimina mvinyo kwenye glasi pamoja na kuwaonyesha kiwango kinachotakiwa. Mafunzo hayo yametolewa kwa muda wa siku tatu katika fani ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Mradi wa SPANEST ambayo yamefungwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ole Sendeka .
ZETE 5
Baadhi ya Wahitimu wa mafunzo katika fani ya ukarimu na Utalii waliochaguliwa na wahitimu wenzao mkoani Njombe ili  kuunda chama chao cha wahudumu wa hoteli, migahawa na nyumba za kulala wageni  kitakachaowasaidia katika kurekebishana na kupaza sauti zao  katika utoaji huduma bora kwa watalii.
ZETE 6
Mmoja  kati ya  Washiriki wa mafunzo  katika fani ya Ukarimu na  Utalii  akitoa nenpo la shukurani ya mafunzo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na mradi wa SPANEST  kabla ya Mgeni rasmi kufunga jana  mafunzo katika fani ya ukarimu na Utalii.
ZETE 7
Mratibu Msaidizi  wa Mradi wa SPANEST nchini,   ( wa kwanza kushoto) akizungumza jinsi walivyojipanga katika kuhakikisha Sekta ya utalii inakua kwa kasi kwa kuwapa mafunzo  wahudumu wa hoteli, nyumba za kulala wageni na migahawa katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika jana Mkoani Njombe kwa muda wa siku tatu.
…………………
Serikali kupitia Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ole Sendeka amesema raia wa Kenya na Uganda wataendelea kuajiriwa katika hoteli zetu kama Watanzania hawataweza kubadilika kwa kuachana na tabia sizizofaa ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na watalii wengi wanaofikia katika hoteli hizo.
Amesema baadhi ya wafanyakazi katika hoteli hizo wamekuwa na tabia za udokozi, uvivu na kiburi akitolea mfano amesema unaweza ukafika katika hoteli ukakaa zaidi ya nusu saa bila kusikilizwa huku wahudumu wakikupita tu kana kwamba hawajakuona, hali inayochangia kwa watalii wanaotembelea vivutio vya utalii kwa mara ya kwanza kutokurudi tena.
 Akizungumza jana wakati akifunga mafunzo yaliyofanyika kwa muda siku tatu mkoani Njombe kwa wahitimu 90 katika fani ya ukarimu na Utalii, alisema ni lazima wabadilike kwa kufanya kazi kwa kujituma pasipo kusimamiwa na mameneja wa hoteli hizo  la sivyo wataendelea kulalamika huku nafasi zao zikiendelea kuchukuliwa na wageni
Amesema wamiliki wengi wa hoteli wamekuwa wakipenda kuajiri wafanyakazi kutoka nchi hizo kutokana na uchapakazi wao na si kwa ajili ya wanajua lugha ya  kiingereza ‘’Wamiliki wananchohitaji ni kupata faida na sio kung’ang’ania kuajiri wazawa ambao hata kumkaribisha mgeni  kwa bashasha imekuwa ni  shida’’ alisisitiza Sendeka
Kufuatana na hali hiyo, amewataka wahitimu wa  mafunzo hayo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji na upishi wakawe chachu katika kuchochea na kuendeleza utalii nchini.
Naye, Mkurugenzi Msaidizi  wa Idara ya Utalii, Paskasi Mwiru amesema mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika nchi nzima baada ya kugundua kuwa  kuna idadi kubwa ya wafanya kazi katika eneo hilo ambalo ni muhimu katika tasnia ya utalii  ni watu wenye ujuzi wa viwango vya chini na baadhi yao hawajapitia mafunzo kabisa.
Alisema kumekuwa na vyuo vya utalii vinavyoibuka kama uyoga na vimekuwa vikizalisha wahitimu wenye ujuzi mdogo hali inayochangia kurudisha nyuma jitihada za serikali za kuongeza idadi ya watalii wanotembelea vivutio vyetu vya utalii.
Kwa upande wa Mratibu Msaidizi wa Mradi wa SPANEST, Edmund Murashani  alisema mradi huo umeamua kujikita katika kuwezesha wahudumu wa hoteli, migahawa na nyumba za kulala wageni wanapata mafunzo kwa kuwa wao ni mojawapo ya nguzo muhimu katika kuhakikisha utalii unakua katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
 ‘’ Tunataka mtalii akifika katika hoteli hizo kitu cha kwanza kabla  hajatembelea vivutio vya utalii vinavyopatikana katika ukanda huo awaze kuongeza siku za kulala katika hoteli zetu kutokana na huduma stahiki anazopata kutoka kwa wahudumu hao’’ Murashani alisema
 Naye, Mhitimu wa Mafunzo hayo, Tulizo Sanga aliomba siku za mafunzo hayo ziweze kuongezwa kwani siku tatu hazitoshi kutokana na umuhimu wa mafunzo hayo kwao.
Mafunzo kama hayo yanatarajiwa kufanyika mkoani Iringa na Songwe chini ya Usimamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia Mradi wa SPANEST unaotekelezwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: WATANZANIA WAASWA KUBADILIKA LA SIVYO WAKENYA NA WAGANDA WATAENDELEA KUAJIRIWA KATIKA HOTELI ZETU
WATANZANIA WAASWA KUBADILIKA LA SIVYO WAKENYA NA WAGANDA WATAENDELEA KUAJIRIWA KATIKA HOTELI ZETU
https://2.bp.blogspot.com/-oJJ2oJEhph4/WNII7hfR_uI/AAAAAAAAYYg/ITgk7s5RAnAgu4swu_OPMGbDXkV4yPn2ACLcB/s1600/ZETE.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-oJJ2oJEhph4/WNII7hfR_uI/AAAAAAAAYYg/ITgk7s5RAnAgu4swu_OPMGbDXkV4yPn2ACLcB/s72-c/ZETE.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/03/watanzania-waaswa-kubadilika-la-sivyo.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/03/watanzania-waaswa-kubadilika-la-sivyo.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy