WATU 22 MBARONI SUMBAWANGA, VITA DHIDI YA MIHADARATI

Sumbawanga. Baada ya msako maalumu wa watuhumiwa wa  dawa za kulevya, watu 22 wamekamatwa mkoani Rukwa wakituhumiwa  kulima, kuuza  na kusafirisha dawa hizo.
Polisi mkoani hapa walisema msako huo uliofanyika hivi karibuni katika wilaya zote na kusimamiwa  na kamati za ulinzi na usalama, mashamba ya bangi  yenye ukubwa  wa heka 19 yameteketezwa,  kilo 15  na misokoto 105 ya bangi imekamatwa. Pia, bila kutaja uzito wake walisema walikamata heroine iliyokuwa ikisafirishwa kutoka Mbeya kwenda Sumbawanga Mjini.
Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi  mkoani Rukwa, Mtatiro Nyamhanga alitangaza vita dhidi ya dawa za kulevya na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa kwenye mamlaka husika.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Julieth Binyura alithibitisha  kukamatwa  watu watano kwa  tuhuma za kumiliki mashamba ya bangi yenye ukubwa wa ekari saba iliyochanganywa na mahindi katika Kijiji cha Ngoma, Kata ya Katete inayopakana na nchi ya Zambia.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post